SHEHE WALID ASEMA TUME IMEJIBU HOJA NYINGI
Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omari amesema Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Vurugu za Oktoba 29 imejibu hoja nyingi zilizokuwa zikihojiwa na Watanzania.Amesema tume hiyo imeleta mambo mazuri ambayo wananchi walikuwa wakiyatarajia, hivyo matokeo yake yanapaswa kutazamwa kama sehemu ya kujenga taifa lenye mshikamano zaidi.
Shehe Walid amesisitiza kuwa ni muhimu viongozi wa dini kuyahubiri mafunzo yaliyotokana na kazi ya tume hiyo kwa waumini wao ili kusaidia kujenga upya Tanzania imara, yenye umoja na amani.
Kwa mujibu wake, taasisi za dini zina nafasi kubwa katika kuhimiza maridhiano, maadili na utulivu wa jamii baada ya matukio yenye kuleta taharuki.
Ameongeza kuwa ushirikiano wa wananchi, viongozi wa dini na taasisi mbalimbali ni msingi wa kudumisha amani na kuendeleza maendeleo ya taifa.

Post a Comment