KIGOMA YAWAKATAA WANAOCHOCHEA VURUGU


Viongozi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) mkoani Kigoma, wamesema uvunjifu wa amani unachangia kuchelewesha au kusitisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.

Kutokana na hali hiyo wameomba wananchi waendelekuwa watulivu wajiepushe na vitendo vya vurugu, huku wakiwapinga wote wanaochochea uvunjifu wa amani nchini.

Wametoa kauli hiyo katika mkutano wao wa pamoja kujadili ushirikiano na namna ya kufanya kazi na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi na kueleza kuwa mazingira ya amani na utulivu ni msingi muhimu unaowezesha mashirika kutekeleza majukumu kwa ufanisi.

Justine Jackson ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Restless Development Tanzania, amesema migogoro na vitendo vya vurugu husababisha ugumu kuwafikia walengwa, kuongezeka kwa gharama za utekelezaji wa miradi na wakati mwingine kusababisha baadhi ya shughuli kusimamishwa kabisa.

Kwa upande waku Mratibu wa miradi wa Shirika la Care Tanzania, Gideon Donalt ameeleza kuwa miradi inayohusu afya, elimu, maji, kilimo, uwezeshaji wa wanawake na vijana kiuchumi pamoja na huduma za kijamii zinahitaji hali ya amani na utulivu katika utekelezaji.

Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NACONGO), Jasper Makala viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali hukutana na kukaa pamoja kujadili changamoto mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao.

No comments