TPA YANUNUA BOTI YA DORIA
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imenunua boti mbili za kisasa za doria, MV LINDO I na MV LINDO II, zenye thamani ya dola za Marekani milioni 6.445, kwa lengo la kuimarisha usalama wa bandari, meli na shehena za wateja katika Bandari ya Dar es Salaam na bandari za Ziwa Victoria.
Boti hizo zina uwezo wa kukimbia kwa kasi ya knots 35, hali itakayowezesha kufanya doria za haraka, kukabiliana na matukio ya dharura pamoja na kudhibiti vitendo vya wizi, udokozi na magendo katika maeneo ya bandari na fukwe zake.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mkurugenzi wa Huduma za Meli na Shughuli za Kibandari, Nahodha Abdulla Mwingamno, amesema uwekezaji huo unaonyesha dhamira ya TPA ya kuhakikisha bandari za Tanzania zinaendelea kuwa salama, zenye ufanisi na zinazokidhi viwango vya kimataifa.
Amesema kuimarika kwa usalama kutaimarisha imani ya wafanyabiashara na wadau wa usafirishaji, kuongeza shehena zinazopita bandarini, kuboresha utoaji wa huduma na kuongeza mapato ya TPA pamoja na makusanyo ya Serikali.
Mbali na ununuzi wa boti hizo, TPA inaendelea kuimarisha usalama kwa kuwekeza katika teknolojia ya kisasa, ikiwemo mfumo wa ufuatiliaji kupitia zaidi ya kamera 480 za CCTV, ili kuhakikisha bandari za Tanzania zinakuwa salama, shindani na zenye uwezo wa kuhudumia ukuaji wa biashara ya ndani na kimataifa.
%20imenunua%20boti%20mbili%20za%20kisasa%20za%20doria,%20MV%20LINDO%20%20(1).jpg)
%20imenunua%20boti%20mbili%20za%20kisasa%20za%20doria,%20MV%20LINDO%20.jpg)
Post a Comment