WATANZANIA WATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI KUFIKIA MALENGO YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050



Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, amewataka Watanzania kuongeza uzalishaji na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ili kuiwezesha nchi kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwani sio mlima mfupi, ikiwemo kufikisha pato la mtu mmoja mmoja dola za Marekani 7,000 na pato la taifa kufikia dola trilioni moja.


Akizungumza na wananchi wa Tarime Mjini mkoani Mara, Dk Nchemba amesema serikali inaendelea kufanya mageuzi ya sheria na mifumo ya utawala ili kuweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji. 
Amesema miongoni mwa maboresho hayo ni kuwapa wafanyabiashara wapya kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kuanza kulipa kodi, badala ya kuanza mara tu wanapoanzisha biashara.

Aidha, amesema serikali imeongeza asilimia tano kwenye mfuko wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya halmashauri na kufikisha asilimia 15, ambapo fedha hizo za nyongeza zitalenga kusaidia wafanyabiashara kuboresha miundombinu na mazingira ya kufanyia biashara.

No comments