JAB Yasogeza Huduma za Usajili na Vitambulisho vya Waandishi wa Habari Kwenye Maonesho ya Sabasaba
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imepiga kambi katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa dhima yake ya kupeleka huduma karibu zaidi na wahitaji.
Banda la bodi hiyo lipo katika Kijiji cha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Bodi hiyo,wadau wa sekta ya habari na wananchi wanaohitaji elimu na huduma zinazotolewa na Bodi hiyo wanaombwa kufika kwa wingi katika banda hilo kwa ajili ya kukamilisha mahitaji mbalimbali ya kisekta.
Aidha Bodi imewakumbusha waandishi wa habari na wadau wote wa sekta hiyo kutumia fursa ya maonesho ya Sabasaba kupata huduma hizo kwa haraka na ukaribu.
Huduma zinaztolewa makao makuu ya Bodi zimepeleka SabaSaba ili kuhakikisha kila mdau anafikiwa kwa wakati.
Ikubukwe kuwa JAB ipo hapo kwa ajili ya kutekeleza jukumu lake la kisheria la kusimamia na kuratibu weledi wa wanahabari nchini .
Huduma zinazotolewa katika maonesho hayo ni pamoja na ugawaji wa vitambulisho vya ithibati kwa waandishi waliokidhi vigezo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229.
Aidha, maafisa wa bodi hiyo waliopo bandani hapo wanashughulikia usajili wa waandishi wa habari, marekebisho ya taarifa zao, pamoja na kutoa elimu kuhusu majukumu na huduma zinazotolewa na JAB.




Post a Comment