HABARI MAALUM: Jeuri ya Tanzania na vita vya kiuchumi vya Tanzania
Matukio yaliyovuta hisia za dunia hivi karibuni nchini Tanzania si matukio ya pekee. Bali ni mlipuko wa vita ya miaka minane (2017–2025) ya kijiografia-kisiasa na kiuchumi, iliyoanza pale taifa hili lilipothubutu kuandika upya sheria za umiliki wa rasilimali.
♟️ Ubao wa Kimataifa wa Kuchezea Sataranji
(chesi)
Tanzania
haikabiliwi tu na mgogoro wa ndani, bali inajikuta imenaswa katika vita ya
kiuchumi-kijiografia (geo-economic war) ya hatari kubwa ambayo imekuwa
ikifunuka kama mchezo kwenye ubao wa kimataifa wa kuchezea sataranji tangu
mwaka 2017. Vita hii haipiganwi kwa silaha za kawaida, bali kwa shinikizo la
kiuchumi, mikakati ya kidiplomasia, na vita iliyoratibiwa ya kidijitali.
Mivutano
ya sasa, iliyofikia kilele chake katika matukio ya Oktoba 29, 2025, ni mlipuko
wa shinikizo lililojengeka kwa miaka kadhaa (2017, 2021 ,2023 , 2025).
⚖️ Mabadiliko Yasiyotarajiwa ya Mwaka
2017
Chanzo
cha mgogoro huu kiko mwaka 2017, mwaka ambao Tanzania ilitekeleza kile
kilichoitwa "kisichowezekana" ("the unthinkable").
Bunge lilipitisha sheria mbili za kimapinduzi ambazo kimsingi ziliipinga sekta
ya uchimbaji wa madini duniani:
- Sheria ya
Umiliki wa Kudumu wa Rasilimali Asilia (2017).
- Sheria ya
Mapitio na Majadiliano Upya ya Mikataba ya Rasilimali Asilia (2017).
Kimsingi,
sheria hizi zilitangaza kwa ulimwengu: "Madini yetu. Masharti yetu.
Uhuru wetu. Nukta." Hatua hii ilionyesha kwa kampuni kubwa za
uchimbaji kuwa Tanzania haikuwa tena "uwanja wa kuchezea" waliouzoea,
ikisisitiza kuwa kampuni za kigeni zingefanya kazi chini ya "sheria mpya.
Sheria zetu."
Rais
Magufuli aliita waziwazi msimamo huu wa kisera kama "Vita ya
Kiuchumi," akisisitiza kuwa nchi ilikuwa imeingia kwenye uwanja wa
vita ikipambanisha madini dhidi ya mataifa makubwa, na uhuru dhidi ya tawala za
zamani.
🌪️ Kisasi na Simulizi
Mbadala
Kisasi
kilikuwa cha haraka. Kwanza, ilianza kuzinduliwa simulizi mbadala ya haraka
katika anga za kimataifa. Wakati masuala kadhaa ya ndani yalikuwepo, simulizi
iliyodai kuwa "Tanzania inafuata mfumo wa kiimla," "Uhuru wa
vyombo vya habari unapungua," na "Upinzani unapungua"—pia ilikuwa
ni shinikizo kubwa la kimataifa. Ujumbe katika hili ulikuwa wazi: huwezi
kuandika upya mikataba ya rasilimali yenye thamani ya mabilioni bila kukabiliwa
na kisasi cha mabeberu wawekezaji hawa.
🤝 Utulivu Kabla ya
Dhoruba (2021)
Kufuatia
mpito wa uongozi mwaka 2021, Rais mpya alichukua msimamo mtulivu zaidi,
ulioambatana na tabasamu la kidiplomasia, kupeana mikono, na kukumbatiana.
Serikali za Magharibi hapo awali ziliamini dhoruba ilikuwa imepita. Hata hivyo,
utulivu huu wa kidiplomasia waliouona ulikuwa wa kupotosha kwani aliyeingia pamoja
na utulivu waliouna aliendelea na mpango wa taifa.
Miradi
miwili ya kimkakati ya rasilimali ilikuwa ikijenga hatma ya muda mrefu ya
Tanzania, hatimaye kupandisha sana joto la kimataifa:
- Mkuju Uranium.
- Lindi LNG.
☢️ Sumu ya Uranium: Urusi Yaingia Kwenye
Kinyang'anyiro
Mradi
wa uranium wa Mkuju si tu operesheni nyingine ya uchimbaji; una moja ya akiba
kubwa na muhimu ya kimkakati za uranium duniani. Katika mazungumzo mengi
, mradi huo haukupewa mataifa ya Magharibi kama Marekani au Ufaransa, bali
ulipewa Rosatom, shirika la Serikali ya Urusi linaloshughulikia masuala ya
nyuklia.
Mshangao
wa kisiasa ulizidi mnamo Julai 31, 2025, wakati Tanzania na Urusi zilipozindua
rasmi kiwanda cha majaribio cha kusindika uranium pale Mkuju. Kwa upande wa
Mataifa ya Magharibi, hii haikuonekana
kama biashara tu, bali kama tishio la kiusalama, ikizingatiwa kuwa
uranium inahusiana na uwezo wa nyuklia, wakaona kuwa Urusi sasa inaidhibiti
akiba ya uranium iliyopo ambayo Tanzania ipo nafasi 10 za juu duniani.
⛽ Bomu la Pili: Gesi na Kuelekea
Mashariki
Suala
kuu la pili la mzozo lilikuwa mradi wa Lindi wa gesi LNG. Makampuni
makubwa ya Magharibi (Shell, Equinor, ExxonMobil, n.k.) yalikaa miaka mingi
kujadili mkataba kuhusu gesi hii (2018–2023) bila mafanikio. Hata hivyo, hali
ilibadilika ghafla wakati maslahi yalipoibuka baada ya mataifa ya Mashariki na
Ghuba, yaani China, Mataifa ya Ghuba, na Gazprom ya Urusi vikionesha nia
ya kuingia katika mradi huo mkubwa wa gesi.
Sasa
unauona mnyororo huo—Uranium inaenda Urusi; Gesi inaenda China/Ghuba/Urusi; kwa
hiyo Diplomasia sasa inaelekea Kuegemea Mashariki na maana yake ni dhahiri
kwamba msingi wa uhuru wa rasilimali ulioanzishwa mwaka 2017 ulibaki imara. Hii
ilifanya ifikiri upya: " Hee kumbe hakuna kilichobadilika tangu
2017?"
📱 Uwanja wa Vita wa
Kidijitali
Kwa
kuona mbinu za jadi za kubanana kiuchumi zinakosa nguvu, mgogoro waliuhamisha
kwenye uwanja wa vita vya kidijitali, ambapo vita vya kisasa hupigwa kwa usambazaji
wa taarifa potofu, huku matumizi yakiwa ni alama za reli (hashtags),
"bots," na simulizi zilizolipiwa ili kuleta mtafaruku.
Tanzania
inaumizwa hapa kwani imetoa uwanja kamili wa vita kwa operesheni za
kisaikolojia kutokana na udhaifu wa ndani katika nyanja tatu:
- Idadi kubwa ya
vijana waliokata tamaa.
- Kizazi cha siasa
kinachotegemea 100% mtandao.
- Vikundi vya
ndani vya kisiasa vyenye njaa ya kupata faida.
Kuanzia
2023 kuendelea, joto la mtandaoni lilipanda haraka isivyo kawaida, likichochewa
na ajenda mbalimbali, kauli za kidini zikipata uzito wa kisiasa, na mgawanyiko
wa kila siku.
Kipindi
chote presha ilikuwa kubwa lakini Tangazo la Mkuju la Julai 31, 2025,
lilitumika kama tamko thabiti, kubwa, na la kiishara kuhusu mwelekeo mpya wa
Tanzania. Miezi mitatu baadaye, mnamo Oktoba 29, valvu ya shikizo la ‘jiko’
na kulipuka.
Tukio
la Oktoba 29 halikuwa "la bahati mbaya" au "la ghafla";
ilikuwa ni mtririrko wa mambo katika miaka minane ya mvutano wa kisiasa.
Tanzania, badala ya kuwa katika mgogoro rahisi wa ndani, inasalia kuwa kipande
muhimu kwenye ubao wa kimataifa wa kuchezea chesi, watu wanataka madini kwa bei
ya kutupa wao ndio wawe wadhibiti.

Post a Comment