RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO YA MUUNDO WA WIZARA , ATEUA VIONGOZI

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko makubwa ya muundo katika Wizara mbili na kuteua viongozi mbalimbali kuziba nafasi zilizo wazi na kuimarisha utendaji serikalini.

Katika mabadiliko hayo yaliyotangazwa leo Februari 06, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji pamoja na Wizara ya Nishati sasa zitakuwa na Makatibu Wakuu wawili kila mmoja.

Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa
  • Kanali Yahya Ramadhani Kido: Ameweuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, akichukua nafasi ya Bi. Fatma Mwassa.

  • Kanali Donald William Msengi: Ameweuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, akichukua nafasi ya Kanali Patrick Kenan Sawala ambaye atapangiwa majukumu mengine.


Makatibu Wakuu na Mabadiliko ya Wizara

  • Dkt. Tausi Mbaga Kida: Ameweuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango.

  • Dkt. Fred Matola Msemwa: Ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Uwekezaji.

  • Balozi Waziri Rajab Salum: Ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara, akichukua nafasi ya Dkt. Hashil Twaib Abdallah.

  • Dkt. James Peter Mataragio: Ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati (Mafuta na Gesi Asilia).

  • Mhandisi Felchesmi Jossen Mramba: Ataendelea kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu).

Makatibu Tawala wa Mikoa (RAS)

  • Dkt. Toba Alnason Nguvila: Ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, akichukua nafasi ya Bw. Missaile Musa aliyestaafu.

  • Dkt. Stephen Justice Nindi: Ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, akichukua nafasi ya Bi. Judica Omary aliyestaafu.

Naibu Makatibu Wakuu

Rais ameteua na kuhamisha Naibu Makatibu Wakuu kama ifuatavyo:

  • Bw. Nsubili A. K. Joshua: Wizara ya Fedha (Huduma za Hazina).

  • Bw. Aristides Robert Mbwasi: Wizara ya Viwanda na Biashara.

  • Prof. Mohammed Sheikh: Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi).

  • Dkt. Fabian Magawa Madele: Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo).

  • Bi. Rose Zacharia Ambrose: Wizara ya Maji.

  • Bw. Emmanuel Tayari: Wizara ya Afya (Dawa na Vifaa Tiba).

  • Prof. Peter Lawrence M. Msoffe: Amehamishwa kwenda Wizara ya Kilimo (Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula).

  • Balozi Baraka Haran Luvanda: Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

Uteuzi mwingine

  • Bw. Sosthenes Laurent Kewe: Ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Taifa ya Mipango.

  • Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti: Ameteuliwa kuwa Balozi.

  • Dkt. Hassan Mahmoud Mshinda: Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Taarifa hiyo imehitimisha kwa kueleza kuwa uapisho wa viongozi hawa wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

No comments