Revocatus Makaranga afariki dunia

 Mwandishi na mhariri mkongwe nchini,Revocatus Makaranga, amefariki dunia  tarehe 5, Machi 2026  mara tu alipofikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa ndugu wa karibu, Makaranga alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwenye kitengo cha dharura kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Hata hivyo, licha ya jitihada za madaktari kumhudumia, amefariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini.

Marehemu Revocatus Makaranga anatajwa kuwa mmoja wa waandishi na wahariri wakongwe nchini waliotoa mchango mkubwa katika tasnia ya habari nchini Tanzania. Makaranga mbali na kufanya kazi katika vyombo vya habari vya umma wakati wa mfumo wa chama kimoja na baadaye vyama vingi, pia alifanya kazi katika kampuni za binafsi za habari za Mwananchi Communications Ltd (MCL), New Habari Ltd . Makaranga ni mhitimu wa shahada ya uzamili katika uandishi wa habari kutoka Chuo Kikuu cha Cardiff, Wales, Uingereza.

No comments