Uzuri wa Tanzania ni Fursa kwa Vijana Kujenga Maendeleo na Ushirikiano




Vijana wa Tanzania wametakiwa kugeuza uzuri na utajiri wa nchi yao kuwa chimbuko la kuanzisha na kujenga mahusiano yenye maana na tija kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla. Kauli hii inatokana na msemo wa Kiingereza unaosema, "Let her beauty be the starting point of meaningful connections."

Wataalamu wa maendeleo ya vijana na viongozi wa jamii wanasisitiza kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi kuanzia vivutio vya utalii, ardhi yenye rutuba, amani na utulivu, mambo ambayo yanapaswa kutumika kama daraja la kuwaunganisha vijana.

Badala ya uzuri wa nchi kutazamwa tu kwa jicho la kitalii na kwa kupewa taarifa za kweli katika upotofu, vijana wanahimizwa kuutumia utajiri huu wa kiasili na kiutamaduni ili kusonga mbele.

Wataalamu hao wanasema kwamba vijana wanaweza kutumia fursa za kimaumbile za nchi (kama vile kilimo, utalii, na madini) kuanzisha ushirikiano wa biashara na miradi ya pamoja. Mahusiano haya yanapaswa kuwa ya kujenga na kuongeza thamani kiuchumi.

" Utamaduni tajiri na wa kipekee wa Tanzania unapaswa kuwafanya vijana wajisikie fahari na kuungana zaidi. Mahusiano ya kijamii yanapaswa kujengwa kwa msingi wa upendo, amani, na kuheshimiana, licha ya tofauti zao za kikabila au kidini." 

Aidha vijana wanatakiwa kuepuka mahusiano ya kindugu au yale yasiyo na tija yenye nia ovu dhidi ya taifa lao na badala yake waelekeze nguvu zao katika kujenga mahusiano ya kitaaluma, kijamii, na kisiasa yanayochochea maendeleo endelevu na ubunifu kwa kutumia teknolojia zilizopo za mawasiliano.

Kiongozi mmoja wa asasi ya vijana amesema, "Uzuri wa Tanzania unapaswa kutukumbusha kwamba sisi ni ndugu. Tunapojenga mahusiano mazuri baina yetu, tunajenga mtandao ambao utatuwezesha kupata masoko, mitaji, na maarifa ya kusaidiana kimaisha."

Kwa kutumia amani na utulivu uliopo nchini, vijana wa Tanzania wanahimizwa kuona uzuri huu wa nchi kama hatua ya kwanza katika kuimarisha umoja na mshikamano ambao ndio kiini cha maendeleo yote.

Hivi karibuni Waziri wa Maendeleo ya Vijana, Dkt. Joel Nanauka,akiwa katika ziara ya mikoa kadhaa nchini kuwasilikiliza vijana, amewataka vijana nchini kutumia utajiri na uzuri wa Tanzania kama chimbuko la kujenga mahusiano yenye maana na tija. 

Akizungumza  maeneo mengi  amewaasa vijana kutumia amani na fursa za kimaumbile za nchi kuanzisha ushirikiano wa biashara na miradi ya pamoja. 

"Badala ya kila kijana kujifungia kivyake, ni wakati sasa wa kuutumia uzuri wa nchi yetu na amani iliyopo kuunda mitandao imara ya kitaaluma, kijamii na kiuchumi. Mahusiano haya ndiyo yatawafanya vijana wawe wabunifu, wapate masoko, na hatimaye kukuza uchumi wetu," alisema Waziri Nanauka.

Akizungumzia utekelezaji wa wito huo, Sophia Mussa, kijana mjasiriamali anayejishughulisha na usafirishaji wa mazao ya kilimo katika Mkoa wa Morogoro, amethibitisha umuhimu wa kushirikiana:

"Mimi nimetumia mitandao ya vijana wajasiriamali niliokutana nao kwenye vikao vya Serikali. Bila amani na ushirikiano, nisingeweza kufikisha mazao yangu Dar es Salaam. Mahusiano tuliyojenga kupitia fursa za nchi yametufanya tuwe na nguvu kubwa ya kiuchumi."

Kwa kutumia amani na utulivu uliopo nchini, vijana wa Tanzania wanahimizwa kuona uzuri wa nchi kama hatua ya kwanza katika kuimarisha umoja na mshikamano ambao ndio kiini cha maendeleo yote. Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuweka mazingira mazuri ya kisheria na kiuchumi ili kuhakikisha vijana wanapata nafasi za kujiajiri na kuajiriwa, huku ushirikiano baina yao ukionekana kuwa kiungo muhimu cha kuendelea mbele.


No comments