Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, September 7, 2013

USAJILI WA MBWEMBWE AMBAO HAKUFUA DAFU ULAYA



LONDON, England

DIRISHA la usajili wa ligi mbalimbali duniani ulifungwa rasmi mwanzoni mwa wiki hii, ambapo ilishuhudiwa timu za Tottenham na Real Madrid zikiongoza katika kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyake.

Katika usajili huo timu hizo kila moja imetumia zaidi ya pauni milioni 100, kwa ajili ya kujiimarisha.
Lakini katika usajili huo, haukuzidisha wachezaji zaidi ya saba wa kimataifa akiwamo nyota, Erik Lamela.
Kwa upande wa Spurs, mashabiki wa timu hiyo wanajivunia kuona sura mpya zikitua kwenye klabu hiyo ya White Hart Lane, licha ya kufungwa na Arsenal katika mtanange uliozikutanisha timu hizo pinzani katika ukanda wa Kaskazini mwa Jiji la London uliopigwa Jumapili iliyopita, wamebaki wakijiamini kushika nafasi ya juu kwenye msimamo wa  Ligi Kuu.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa matumizi mengi ya fedha mara zote hayawezi kukupa uhakika wa kufanya vizuri na kwa kutumia fedha nyingi kwenye usajili unaowasajili kwa bei mbaya wanaweza wasifanye vizuri.
Ifuatayo ni orodha ya timu  na wachezaji waliosajiliwa  kwa gharama kubwa, lakini wakashindwa kuonesha viwango vyao.
1.Chelsea 2006/07-Pauni miliono 83.5

Timu ya Chelsea ilijikuta ikitumia pauni milioni 83.5, ili kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya kutwaa ubingwa wake wa Ligi Kuu.

Huku Manchester United na Arsenal zikiwa nyuma yake, Chelsea ilikuwa na uhakika ingeweza kutwaa ubingwa wa tatu mfululizo wa ligi hiyo.

Kama ilivyokuwa misimu iliyopita wakati wa usajili huo, kibopa wa timu hiyo, Roman Abromovich alifungua tena kitabu chake cha benki kwa ajili ya kusaka ubingwa wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, ambapo katika usajili huo, tajiri huyo mkubwa alijikamua pauni milioni 30 ili kuhakikisha  anamnasa mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ukraine, Andriy Shevchenko usajili ambao ulionekana kuwa wa kufuru kwenye michuano ya Ligi Kuu ya England.

Hata hivyo, Sevchenko alishindwa kufanya kweli na badala yake akajikuta akifunga mabao tisa tu katika mechi 48 alizoichezea timu hiyo kabla ya kurejea AC Milan kwa mkopo miaka miwili baadaye.

Inaelezwa kushindwa kutamba mchezaji huyo, ndicho kilichoifanya timu hiyo kupoteza ubingwa kwa Manchester United ambayo iliwazidi kwa pointi sita.

Hata hivyo iliweza kutwaa ubingwa wa Kombe la Ligi na Kombe la FA, lakini ubingwa wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya ikausikia bombani.

Wachezaji wengine ambao iliwanunua msimu huo ni Salomon Kalou kwa pauni mil 3.5, Jon Obi Mikael, pauni mil 16 na Khalid Boulahrouz ambaye ilimnunua kwa pauni mil 6.

 2.Manchester United  2001/02 –Pauni milioni 75.5

Kutokana na kupata matokeo mabaya misimu iliyopita, ambapo  ilishuhudiwa Man United ikifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara moja, aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson aliamua kufanya matumizi makubwa ili kuimarisha kikosi chake.

Katika usajili huo, mabingwa hao wa sasa wa Ligi Kuu ya England, waliamua kuvunja rekodi ya usajili nchini Uingereza kwa kumsajili nyota wa timu ya Taifa ya Argentina, Juan Sebastian Veron kwa pauni milioni 28.1 akitokea katika timu ya Lazio.Mbali na mchezaji huyo, pia Man United ikaona bado haifai, ikaamua kuvunja tena benki na kuwachukua Diego Forlan na Ruud Van Nisterlooy kwa pauni milioni 6.9 na 19.

Hata hivyo pamoja na kujikamua kitita hicho cha pauni milioni 75, Manchester United ilijikuta ikimaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya mahasimu wao Liverpool  na Arsenal.

Mbali na pigo hilo, timu hiyo ilijikuta ikitupwa nje ya michuano ya Kombe la Ligi kwenye raundi ya tatu, baada ya kupokea kipigo cha mabao 4-0 na Arsenal kabla ya kuchapwa na timu ya Middlesbrough katika raundi ya nne ya michuano ya Kombe la FA.

Pia licha ya kocha Alex Ferguson kuiwezesha timu hiyo kutinga nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, lakini alijikuta akitupwa nje ya michuano hiyo ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen kwa bao la ugenini.

Baada ya kumaliza msimu ikiwa haina ubingwa wowote na huku Veron na Forlan wakishindwa kufurukuta, majaliwa ya Man Utd yalionekana kuwa kitendawili.

 

3.Manchester City 2008/09 – Pauni milioni 140

Katika usajili wa mwaka huo, Manchester City ilitangaza kuingia kwenye matumizi makubwa ya usajili, pale ilipotangaza  dakika za mwisho za usajili wa mwaka 2008 kwa kumnasa Robinho ambaye wakati huo alikuwa akikipiga Real Madrid.

 

Ikisaidiwa na mmiliki mpya wa timu hiyo, Sheikh Mansour, Man City ilivunja rekodi ya usajili nchini Uingereza, kwa kutoa pauni milioni 32.5 ili kuhakikisha inamnasa nyota huyo wa timu ya Taifa ya Brazil ambaye alitarajiwa kusaini Chelsea.

 

Hata hivyo licha ya ukiwa na mchezaji mmoja nyota unaweza kutwaa ubingwa, lakini Man City ilijikuta ikiwa juu ya mstari wa kushuka daraja kwa pointi moja hadi mwaka mpya.

Hali hiyo ndiyo iliyomlazimisha aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mark Hughes kupewa fungu jingine katika usajili wa Januari ambapo aliweza kuwasajili, Nigel De Jong kwa pauni milioni 18, Wayne Bridge kwa pauni milioni 12 na Craig Bellamy ambaye ilimnunua kwa pauni milioni 14.
Kwa ujumla katika usajili huo, Manchester City ilitumia pauni milioni 140, lakini ikajikuta ikimaliza ligi ikiwa kwenye nafasi ya kumi.
Huku ikiwa imeshatumia fedha nyingine kumnunua, Stephen Ireland, ambaye aliibuka mchezaji bora wa  mwaka badala ya Robinho ambaye ilimnunua kwa bei mbaya.
Licha ya kununua wachezaji 13 kwa sasa Vincent Kompany na Pablo Zabaleta  ndiyo wamebaki kwenye kikosi hicho.
Ikiwa ni kama kutokata tamaa, Manchester City iliendelea kumwaga fedha msimu uliofuata, ambapo katika usajili wa mwaka  2009 ilishuhudiwa ujio wa wachezaji, Roque Santa Cruz ambaye ilimnunua kwa pauni milioni 18, Emmanuel Adebayor, pauni milioni 25 Kolo Toure, pauni milioni 16, Carlos Tevez, pauni milioni 25.5 na Joleon Lescott ambaye ilimsajili kwa pauni milioni 24.

Kwa usajili huo Man City ilionekana kuimarika, ambapo aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mark Hughes aliiongoza kushika hadi nafasi ya nne bora kabla ya kufukuzwa kabla ya kufika mwaka mpya na mikoba ya timu hiyo kukabidhiwa kwa Roberto Mancini, lakini naye akashindwa kuitoa kwenye nafasi iliyokuwepo wakati Hughes akifukuzwa.
Kutokota kwa timu hiyo kulionekana zaidi wakati wa mechi ya nusu fainali ya Kombe la Ligi, ambapo ilishuhudiwa ikipokea kipigo cha jumla ya mabao 4-3 kutoka kwa mahasimu wao, Manchester City.
Licha ya kusajili wachezaji nyota kwa mkupuo, lakini kwa sasa mchezaji pekee ambaye amebaki na timu hiyo ni Joleon Lescott ambaye naye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa.

4.Real Madrid 2009/10 – Pauni 225

Katika usajili wa msimu huu, Rais Florentino Perez alitangaza kurejea madarakani kuiongoza Real Madrid, huku akitangaza kufanya kufuru ya matumizi ya fedha kwenye historia ya soka.

Katika kipindi cha usajili huo wa majira ya joto, Real Madrid ilivunja rekodi ya usajili mara mbili kwa kumsajili Kaka kwa pauni milioni 57 na Cristiano Ronaldo kwa pauni milioni 80.

Mbali na wachezaji hao katika usajili huo, kilishuhudiwa kigogo hicho cha soka Hispania kikijikamua pauni milioni 30 kumsajili, Karim Benzem na  ikitoa kiasi kama hicho kwa  Xabi Alonso.
Hata hivyo pamoja na kufanya kufuru hiyo, timu hiyo haikufanya vizuri kwani ilishuhudiwa mahasimu wao Barcelona wakiwapiku kwa kutwaa ubingwa wa ligi ya  La Liga wakiwa na pointi 99 dhidi ya 96, ilizokuwa nazo  Real Madrid

Mbali na hilo la kukosa ubingwa wa ligi ya ndani, timu hiyo ilijikuta ikichemsha kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, baada ya kujikuta ikichapwa na Lyon kwenye raundi ya pili.
Timu hiyo pia ilijikuta ikifedheheka kwenye michuano ya Kombe la Copa del Rey kwa kuchapwa na timu ya Alcorcon, kwa jumla ya mabao 4-1 katika raundi ya 32 yaliyoifanya ibaki bila kuwa na ubingwa baada ya kushindwa kuonesha thamani ya pauni milioni 225 ilizowekeza.

No comments:

Post a Comment