Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, September 7, 2013

KOCHA HODGSON AKERWA NA KADI KWA DANNY WELBECK


Timu ya Taifa ya England jana waliifunga Moldova 4-0 na kujikita kileleni mwa Kundi H la kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwakani lakini Kocha wao, Roy Hodgson, amekasirishwa sana na Refa kutoka Slovakia kwa kumpa Kadi ya Njano Danny Welbeck itakayomfanya aikose Mechi muhimu sana ya Jumanne huko Kiev dhidi ya Ukraine.

Refa Ivan Kruzliak kutoka Slovakia kumpa Kadi ya Njano kwa kuendelea kucheza Mpira na kupiga shuti baada ya kupigwa Filimbi ya yeye kuotea kufuatia Bendera ya Msaidizi wa Refa kuashiria Ofsaidi ambayo hakika haikustahili.
Kocha Roy Hodgson alimvaa Refa wa Akiba na kumpandishia na Sekunde chache baadae Welbeck akaifungia England Bao la tatu na la kwanza kwake.

Mbali ya Hodgson kulalamika, hata Welbeck mwenyewe alimfuata Refa na kulalamika sana kuhusu Kadi ile.

Nae Hodgson alieleza: “Sidhani kama wapo Watu wengi, hata Marefa wenyewe, watakaounga mkono Kadi ile. Hata Kadi ya Njano ya kwanza aliyopewa Welbeck huko Montenegro Mwezi Machi ni uonevu kwani yeye alistahili Penati na si Kadi kwa kujiangusha. Sasa yupo nje Gemu ya Ukraine”

Upungufu huo, pamoja na kuwakosa Wayne Rooney na Andy Carroll, ambao ni Majeruhi, kunamfanya Hodgson amtegemee Jermaine Defoe, ambae nae ndio anarudi toka kwenye maumivu, na Rickie Lambert wa Southampton ambae Jana alicheza vizuri mno na kufunga Bao moja.

Pia upo uwezekano mdogo kwa Straika wa Liverpool, Daniel Sturridge, kusafiri kwenda Kiev ikiwa kesho Jumapili Madaktari watampasisha kupona kwake maumivu ya Paja ambalo yalimfanya Juzi arudi Klabuni kwake Liverpool kwa matibabu zaidi.

MSIMAMO:

KUNDI H








NAFASI Team P W D L F A GD Pts
1 England 7 4 3 0 25 3 22 15
2 Montenegro 8 4 3 1 15 8 7 15
3 Ukraine 7 4 2 1 19 4 15 14
4 Poland 7 2 4 1 13 8 5 10
5 Moldova 8 1 2 5 4 15 -11 5
6 San Marino 7 0 0 7 0 38 -38 0
KUMBUKA:
:WASHINDI 9 WA MAKUNDI WATATINGA MOJA KWA MOJA BRAZIL
:WASHINDI WA PILI 8 BORA KATIKA MAKUNDI 9 WATAPANGIWA MECHI SPESHO ZA MCHUJO ZA MTOANO ILI KUPATA TIMU 4 KUUNGANA NA WASHINDI 9 WA MAKUNDI KWENDA BRAZIL

RATIBA:
Jumanne Septemba 10
San Marino v Poland
Ukraine v England
Ijumaa Oktoba 11
England v Montenegro
Moldova v San Marino
Ukraine v Poland
Jumanne Oktoba 15
England v Poland
Montenegro v Moldova
San Marino v Ukraine

No comments:

Post a Comment