Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, September 7, 2013

DANIEL STURRIDGE ANATAFUTIWA MTAALAM KUMWONGEZEA MBINU ZA MAUAJI





AMEKUWA gumzo kubwa hivi sasa! Ndiyo hii inatokana na uwezo wake mzuri aliouonyesha tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya soka ya England (EPL).

Anazungumziwa Daniel Sturridge mshambualiji chipukizi wa Majogoo wa jiji Liverpool  vijana wa Brendan Rodgers wenye maskani yao kwenye dimba la Anfield. Alionekana kana kwamba ametua Anfield kuikomboa klabu hiyo katika lindi la ubutu wa safu ya ushambuliaji na tangu siku pili ya ya mwaka 2013 alipotua Liverpool akitokea Chelsea.

Msimu huu ameanza kwa kismati, amefunga mabao matatu muhimu katika mechi tatu na kuiwezesha Liver pool kuongoza ligi kwa kuwa na pointi tisa huku bao moja akifunga dhidiya Manchester united katika siku ambayo alikuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Mabao mawili aliyofunga pia kwenye mechi ya kombe la Ligi  inamfanya kuwa mshambuliaji mwenye wastani mzuri zaidi misimu huu kwa kuwa amecheza mechi nne na kufunga mabao matano, na kumfanya kufikisha jumla ya mabao 16 katika mechi 20 alizoichezea Liverpool tangu ajiunge  na timu hiyo mwezi Januari mwaka huu.

Bilahs amwanzo huu umenyesha nyota njema kwa Liverpool na straika huyo chipukizi na amerejesha matumaini makubwa kwa mashabiki kuanza kuziota nafasi za juu za ligi hiyo msimu huu baada ya kuwa nje tha the Big four kwa takriban miaka saba.

Utawaambia nini mashabiki wa Liverpool wakuelewe leo hii juu ya nyota huyo? Ukitaka wakuchukie sasa mchezee rafu au meme vibaya bila shaka hata gazeti au tV yako haitatazamwa kamwe na mashabiki wa vijogoo hao wa Anfield ambao kwa sasa wanajiona kuwa na kikosi bora cha kuwafutia machungu na machozi ya muda mrefu.

Kama ilivyo kwa kocha wao, pia mashabiki wa Liverpool duniani kote wanaamini kwamba Sturridge  atawaburuza washambuliaji wengine kwenye ligi ya EPL msimu huu. Rodgers anaamini Sturridge atakuwa mshambuliaji wa kuogopwa sana katika bara la Ulaya msimu huu.

Nyota huyo Muingereza mwenye asili ya Afrika alizaliwa  katika mji wa Birmingham, September 1, 1989  na alianza soka katika klabu ya kwao ya Aston Villa  kabla ya kuhamia Coventry  na baadaye mwaka 2003 akajiunga na Manchester City.

Pamoja na nyota njema kuonekana kung’ara kwa nyota huyo, kuna mambo kadhaa ambayo anatakiwa kufanya ili afanikiwe kuendelea kung’ara kwenye michuano ya Ligi Kuu na kupachika mabao   zaidi.

Anatakiwa kuendelea kuwa Fiti
Jambo muhimu na la kwanza ni Sturridge kuendelea kuwa fiti katika kiwango alichonacho hivi sasa. Liverpool lazima wahakikishe kwamba nakuwa fiti kiafya ili kuhakikisha wanamtumia dimbani kwanza kwamanufaa ya klabu na manufaa yake kama mshambuliaji, alikuwa akikabiriwa na majuruhi katika msimu uliopita hii itampotezea kasi yake  na pengine  hii itamuondoa mchezoni.
Itakumbukwa kwamba alikosa karibu msimu wote wa maandalizi baada ya kuwa majeruhi mwishini mwa msimu, ameumia kidogo kwenye mechi na Manchester United na hii inamuweka nje ya kikosi cha England kitakachocheza na Moldova katika kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia, ingawa ameelezwa kwamba takuwa fiti kwenye mchezo mwingine dhidi ya Ukraine wiki ijayo.

Kuendeleza kiwango chake
Sturridge amekuwa katika kiwango kizuri mwanzoni mwa msimu, ameonyesha uwezo mzuri katika kutembea na mpira, kujitengenezea nafasi  na kutengeneza nafasi kwa wachezaji wengine uwezo wake katika kunyang’anya mipira na kumiliki ndiyo silaha yake kubwa ambayo anakiwa kuiendeleza.
Tayari msimu huu ameonyesha umahiri wa kucheza na mpira  na kutengeneza nafasi kwake na kwa wenzie, amekuwa mjanja  na mabao yake yote matatu yameonyesha jinsi gani alivyokuwa mjanja katika kujipanga  dhidi ya mabeki.

Matumizi ya mguu wa kulia
Ingawa Sturridge ni mtu wa mashoto, lakini anatakiwa sasa kuutumia vyema mguu wake wa kulia hasa anapokuwa mbele ya mabeki hii itamsadia zaidi  katika kuhama na mipira na hata kupiga mashuti kote kutokea pande zote.

Rodgers ametafuta mtaalam kwa ajili ya kumnoa Sturridge juu ya matumizi ya muguu wa kulia  zaidi anatakiwa kuongezea wepesi na nguvu na akifanikiwa katika hilo bila shaka chipukizihuyo atatisha zaidi barani Ulaya.
Pamoja na hiyo hadi sasa hakuna mwenye shaka na Sturridge hofu zaidi kwa wapinzani lakini kwa Liverpool mioyo imetulia.

No comments:

Post a Comment