Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 5, 2013

MESUT OZIL KUHAMIA GUNNERS, DUNIA YA REAL YAHUZUNIKA. KIONGOZI JOACHIM LOW, CRISTIANO RONALDO, RAMOS WAMLILIA!! MKURUGENZI JORGE VALDANO AWAKA NAE



MENEJA wa Germany Joachim Low ameuelezea uamuzi wa Real Madrid kumuuza Mesut Ozil kwa Arsenal ni kitu kisichoeleweka huku Wachezaji wa Real, akiwemo Cristiano Ronaldo, wakihuzunika na kuondoka kwake.
Jumatatu Usiku, Siku ya mwisho ya Kipindi cha Uhamisho, Arsenal ilivunja Benki na Rekodi yao wenyewe kwa kutoa Kitita cha Pauni Milioni 42.4 kumnunu Kiungo huyo wa Germany mara tu baada ya Real kumsaini Gareth Bale kwa Dau la Rekodi ya Dunia la Pauni Milioni 86.

Ozil kushoto akionesha jezi ya Gunners juu na kulia ni Straikar Lukas Podolski
Mesut Ozil
-Katika Misimu mitatu na Real Madrid, Ozil alisuka Bao 47 kwenye La Liga na yeye kufunga Bao 19.

Lakini Meneja wa Germany Joachim Low amehoji uamuzi wa kumruhusu Ozil kuihama Real.
Amesema: “Kwangu, haieleweki kwa Real kumuuza mmoja wa Wafungaji wao bora. Wachezaji wengi wa Real kama Sami Khedira na Cristiano Ronaldo wamehuzunika na Uhamisho huu.”
Hata hivyo, Kocha huyo wa Germany amegusia kuwa Ozil atanufaika na kuhamia Arsenal kwa jinsi Meneja wa Klabu hiyo, Arsene Wenger, alivyohangaika kumsaini.
Low, ambae yuko na Ozil kwenye Kikosi cha Germany ambacho Ijumaa kinapambana na Austria kwenye Mechi ya Kombe la Dunia, amedai sapoti ya Wenger na staili ya uchezaji ya Arsenal itamsaidia sana Mchezaji huyo.
Nao Wachezaji wa Real wameibuka na kuzungumza kwa huzuni kuhusu Uhamisho wa Ozil.
Nyota wao mkubwa, Cristiano Ronaldo, alitamka: “Yeye alikuwa ndie Mchezaji mkubwa aliejua muvu zangu Uwanjani. Nimekasirika kuondoka kwake!”
Nae Sergio Ramos alisema: “Ni mwenzangu na Rafiki yangu! Ni aibu. Ni Mchezaji bora. Ingekuwa naamua nini kinatokea Real, angekuwa Mtu wa mwisho kuondoka!”
Si Wachezaji tu waliohuzunishwa kuhusu Ozil, hata aliekuwa Mkurugenzi wa Michezo wa Real, Jorge Valdano, amesema: “Kama wangenipa mimi uamuzi, ningeweka mbele ushirikiano wa Ozil-Angel Di Maria kuliko Bale. Hakika ningemweka Ozil mbele ya Bale!”Tribute: Sergio Ramos posted this picture on Twitter of him proudly holding Mesut Ozil's last Madrid shirtSergio Ramos nae kaanika tisheti iliyoandikwa mgongoni Ozil kwenye TwitterStrike a pose: Fellow attacking midfielder Isco was another player to question the sale of OzilIsco amekuwa mchezaji mwingine aliyeumia kuuzwa kwa mchezaji huyo!!!New man: Bale was unveiled as a Real Madrid player after his world-record move from TottenhamOzil ameuzwa baada ya Real Madrid kununua Jembe Bale kwa £86million kutoka TottenhamPinpoint passing: Ozil (centre) in action against Granada's Brayan Angulo (left) and Hassan Yebda
Ozil akitoa pasi wakati wanacheza na timu ya Granada kushoto ni Brayan Angulo na Hassan Yebda

No comments:

Post a Comment