Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 5, 2013

KATIBU MKENYA AGEUKA AGENDA JANGWANI




TAMKO la wazee wa Yanga kuhusiana na kupinga ajira mpya ya Katibu Mkuu kutoka Kenya, Patrick Naggi imeonesha kuwawewesesha viongozi wa klabu hiyo, kufuatia jana Sekretarieti ya Klabu hiyo kukaa kikao kizito kujadili suala hilo, ambapo leo wanatarajia kutoa tamko lao kuhusu sakata hilo.
 
Naggi aliwasili klabuni hapo jumatatu iliyopita, kuchukua nafasi ya Lawrence Mwalusako, ambaye  alikuwa akiikaimu nafasi hiyo kwa muda, baada ya uongozi mpya wa klabu hiyo kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa awali Celestine Mwesigwa.

Akizungumza na leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga alisema hawataki kulumbana na wazee, isipokuwa msimamo kamili wa uongozi kuhusiana na suala hilo watautoa leo.

"Tulitoa tenda kwa Kampuni moja, ambayo ilimpata Naggi aliyekidhi sifa na vigezo, kupitia mchakato  kwa waombaji walioomba ajira hiyo, ambapo uraia siyo kigezo cha kumuondoa huyo, kwani ni nafasi ya kuajiriwa.

"Bado hajaanza kazi rasmi kama inavyoelezwa na alienda klabuni kwa ajili ya kumsalimia Lawrence Mwalusako, ambaye ni rafiki yake wa muda mrefu," alisema Sanga

Alisema atakuwa Katibu rasmi pale tu watakapotoa taarifa za kumtambulisha, lakini sasa bado hajashika madaraka hayo, ambayo yanafanywa na Mwalusako.

Hata hivyo kauli hiyo inapingana na kauli aliyoitoa jumanne iliyopita Katibu wa sasa Mwalusako, ambaye alinukuliwa kwenye vyombo vya habari akisema tayari ameshaambiwa na uongozi wake amkabidhi madaraka Mkenya huyo. 

Ambapo alisema ajira yake hiyo ilikuwa ya muda, wakati viongozi wakiwa kwenye mchakato wa kumpata Katibu mpya.

Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali alitoa tamko juzi jijini Dar es Salaam, ambapo alisema wanapinga ajira hiyo ya Mkenya, kwani katiba yao inataka kiongozi yoyote lazima awe mwanachama waklabu hiyo.

No comments:

Post a Comment