SEPP BLATTER NA DAVID CAMEROON WAMTAKIA HERI FERGUSON
SALAMU kwa watu maarufu
mbalimbali za kumtakia heri meneja wa klabu ya Manchester United, Sir Alex
Ferguson zimeendelea kumiminika mara baada ya kocha huyo kutangaza rasmi
kustaafu mwishoni mwa msimu huu.
Mojawapo ya salamu hizo ni
kutoka kwa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon na Rais wa Shirikisho la Soka
Duniani-FIFA Sepp Blatter ambao kwa nyakati tofauti wamesifu kazi nzuri
aliyofanya huku Blatter akithubutu kusema hapata kuja kutokea kocha wa aina yake
United atakayeipa mafanikio kama ya Ferguson.
Cameroon ambaye ni mshabiki
wa klabu inayosuasua katika Ligi Kuu nchini humo ya Aston Villa yeye aliandika
katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa mafanikio aliyopata
Ferguson akiwa na United ni makubwa akaendelea kusema kuwa anategemea kustaafu
kwake itakuwa ahueni kwa timu yake akimaanisha Aston Villa. Mbali na viongozi
hao lakini pia wachezaji mbalimbali wa zamani wa klabu hiyo akiwemo Paul Ince,
Peter Schmeichel na wengineo nao wameandika katika mitandao yao wakimtakia heri
kocha huyo huku Ince akionya kocha atakayechukua nafasi yake apewe nafasi kama
ilivyokuwa kwa Ferguson wakati ametua hapo mwaka 1986.
David Moyes Kocha wa Everton ambaye anapewa nafasi ya kuchukua ukocha ndani ya masaa 24
Post a Comment