Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Oseah |
Shirikisho
la soka la Tanzania (TFF) ambalo ndilo litakalo kuwa mwenyeji wa mechi ya Tanzania
dhidi ya Uganda June 23 mwaka huu wa kutafuta mabingwa wa nchi za Afrika (Chan) kabla ya kurudiana baada ya wiki mbili
limewasilisha kusudio la kuomba mchezo
huo kuahirishwa kwa Uganda kutokana na Tanzania kukabiliwa na ratiba ya kushiriki
michuano ya COSAFA dhidi ya Mauritius.
Kwa mujibu
wa taarifa ambazo Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF)
Angetile Osiah aliyoitoa kwenye mtandao wa star africa inasema kuwa wamewasilisha ombi lao FUFA lakini inawezekana Uganda
wakakataa kwani bado hawajapata jibu kutoka FUFA la kubadili tarehe ya
mchezo huo.
LENZI YA MICHEZO
ilimtafuta Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kwa simu lakini hakutaka kuweka
wazi kwa sababu ya taratibu za kiofisi
Mashindano
ya COSAFA ambayo Tanzania inashiriki kama mwaliko pamoja na Kenya wakitokea
ukanda wa CECAFA yatashirikisha nchini
14 , ambayo yatafanyika kwenye miji ya Lusaka, Ndola, Kabwe na Kitwe
huko Zambia na Tanzania itafungua dimba na Shelisheli Julai 6, mwaka huu.
Mechi ya pili ya Taifa Stars
katika hatua ya makundi itakuwa Julai 8 mwaka huu dhidi ya Mauritius. Mechi ya
mwisho katika hatua hiyo itakuwa Julai 10 mwaka huu dhidi ya Namibia na
yatafikia tamati Julai 20, mwaka huu
Nchi za
COSAFA zinazoshiriki michezo hiyo ni Swaziland, Namibia, Botswana, Lesotho,
Mauritius na Shelisheli,
Zambia, Afrika ya Kusini, Angola, Zimbabwe, Msumbiji na Malawi
Naye kocha
wa timu hiyo Kim Poulsen amesema kuwa timu yake itacheza mechi ya kirafiki
kabla ya kucheza na Morocco’s June 8, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment