RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA, WANG YI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 10 Januari, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Wang Yi, katika Ikulu ya Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Wang Yi amewasilisha Salamu Maalum kwa Mhe. Rais Samia kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping, ikiwa ni ishara ya kuendeleza na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kirafiki yaliyopo baina ya nchi hizi mbili kwa miongo mingi.
Viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kimkakati, yakiwemo:
Uimarishaji wa miradi ya miundombinu na nishati.
Ukuaji wa biashara na uwekezaji nchini Tanzania.
Ushirikiano katika nyanja za kimataifa kwa maslahi ya pande zote mbili.
Ziara hii ya Mhe. Wang Yi nchini Tanzania inasisitiza umuhimu wa Tanzania kama mshirika mkuu wa China barani Afrika na dhamira ya viongozi hawa wawili katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi.





Post a Comment