LIONEL Messi alifunga mabao 91, mwaka 2012, hii inamaanisha
kwamba kuna wakati kwenye mwaka huo, mabeki 91 walifanywa waonekane wapuuzi
katika kazi yao.
Ndio inajulikana kwamba idadi ya mabeki waliofanywa wapuuzi ni
kubwa kuliko hiyo. Messi anapoingia uwanjani, wachezaji wenzake kwenye timu
yake wanapata ari, wakati mabeki hata kama ni bora duniani wanapata kitete.
Messi ni mfupi, lakini kwenye soka ni bonge la mtu. Akiwa na
miaka 25 tu, tayari anatajwa kama mmoja kati ya wachezaji bora wa kizazi chake
na mmoja kati ya bora wa muda wote.
Inafananaje kukabana na Messi? Hapa inaangaliwa kiufundi
zaidi. Lakini hakuna beki ambaye anaweza kudiriki kusema kwamba kumkaba Messi
ni rahisi, kuna baadhi wamefanikiwa. Katika kujaribu kutafuta jibu la hili
swali, makala haya yameangalia wakati bora na mbovu kwenye maisha ya soka ya
Messi.
Kiufundi
zaidi
Messi alikuwa kabla ya kutengenezwa na kuwa mashine ya
ufungaji chini ya usimamizi wa Pep Guardiola, Barcelona. Akicheza kama namba
tisa wa uongo (False 9), Messi anacheza chini zaidi tofauti na namba tisa wa
kawaida anavyotakiwa kucheza, hii inawapa wakati mgumu sana mabeki wa timu
pinzani kumkaba ‘Man to man’.
Chini ya Guardiola Messi alicheza kati na David Villa kushoto.
Villa alikuwa akiingia kati kati na Messi kukimbilia pembeni, ili kuwachanganya
mabeki. Tito Vilanova aliiga mfumo huu wakati wa mechi ya pili ya hatua ya 16
bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan na matokeo yalikuwa mazuri kwa
Barca.
Barcelona inacheza kumzunguka au kwa kumuangalia Messi, ambaye
ana majukumu madogo sana ya kukaba, ili kumfanya asichoke. Licha ya mfumo pia
uwezo binafsi wa Messi kwenye kumiliki mpira, kasi, kuchanganya haraka akiwa
anakimbia, kuusoma mchezo, kasi ya miguu yake na uwezo mkubwa wa kubadili
mwelekeo.
Kumalizia ni kwamba, Messi anajua kuutumia mguu wake wa
kushoto hivi vyote vinamfanya yeye na Barca kutisha ulimwenguni.
Kutafsiri
mbinu uwanjani
Wakati Chelsea wakijiandaa kukutana na Messi pamoja na Barcelona
kwenye nusu fainali ya ligi ya mabingwa 2011-12, Kocha wa muda wa The Blues na
timu yake Roberto Di Matteo, walihangaika sana kutafuta mbinu sahihi za kuzuia
soka la pasi la Barca. Huku Messi akijadiliwa zaidi.
“Uwezo wake akiwa na mpira ni balaa, lakini cha muhimu zaidi
anaweza kubadilika kadri mechi inavyosonga mbele,” kipa wa Chelsea, Petr Cech alinukuliwa
na gazeti la Daily Telegraph. “Dakika za mwisho katika mazingira yoyote anaweza
kupata suluhisho la tatizo lolote, kuna staili nyingi anaweza kutumia kumalizia
mashambulizi.”
Cech aliongeza: “Kwa upande mwingine, ni mtu wa kawaida kama
wengine, kama tukicheza kwa asilimia 100, tutaweza kujilinda dhidi yake.”
Maneno ya mwisho ya Cech yalikuwa sahihi. Chelsea walimkera Messi
na kuifunga Barcelona kwenye nusu fainali kwenye msimu huo, kabla ya kusonga
mbele na kuchukua ubingwa wakitumia mfumo wa ‘kupaki basi’. Japokuwa unaweza
kusema kuwa bahati ilikuwa yao kwenye msimu huo.
Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora msimu huu, AC
Milan walishinda 2-0 kwenye mechi ya kwanza, San Siro, walicheza soka la
kujilinda zaidi kama Chelsea msimu uliopita. Ushindi huo haukuwasaidia, kwa
sababu kwenye mechi ya marudiano Barca, ikiwa na Messi aliyekuwa kwenye fomu,
iliibuka na ushindi wa mabao 4-0, matokeo ambayo yalimuacha kocha wa Milan, Massimiliano
Allegri akiumwagia sifa ‘Utatu mtakatifu’ wa Barca, Messi, Xavi Hernandez na Andres
Iniesta.
Hapo pia kuna sababu nyingine ambayo inaongeza ugumu kwenye
kumzuia Messi. Timu inawezaje kumzuia Messi na mfumo mzima wa Barca wa pasi na
umiliki wa mpira?
“Ukimuona Iniesta anavyokokota mpira kwa dakika 90 bila
kuchoka, unaweza kugundua vitu vingi sana,” Allegri alinukuliwa na gazeti la The
Independent. “Ni moja ya timu ngumu zaidi duniani na wana wachezaji watatu wa
kipekee Messi, Xavi na Iniesta."
Zaidi ya
mbinu
Messi ana mchango mkubwa Barca ambao hata mtaalamu wa kawaida
hawezi kuuelezea. Kwenye msimu huu wa ligi ya mabingwa, Messi alipata majeruhi
kwenye mechi ya kwanza ya robo fainali dhidi ya Paris Saint-Germain. Kwenye
pambano la Nou Camp alianzia benchi, aliingia uwanjani kipindi cha pili wakati
timu yake ikiwa nyuma kwa bao 1-0.
Mara baada ya kuingia uwanjani, mechi ikabadilika. Uwepo wa
Messi ulionekana kuongeza ari kwa wachezaji wengine wa Barcelona. Barca
walipata bao dakika chache tu, baada ya Messi kuingia wakapata sare ya 1-1
wakaenda nusu fainali.
Wote Barca na PSG walibadilika baada ya Messi kuingia
uwanjani, hii ni kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la England.
Baada ya filimbi ya mwisho Villa alisema: “Messi ni mchezaji
bora wa dunia, na alibadilisha kila kitu kwa uwepo wake uwanjani.” Alinukuliwa Villa
na gazeti la Daily Telegraph. Wakati kocha wa PSG Carlo Ancelotti yeye alisema:
“Ni wazi Messi aliwaongezea kujiamini timu yake, kwa sababu hata kama hayuko
fiti asilimia 100 bado ni mchezaji wa kipekee.”
Katika hili, mbinu na kipaji havikuwa muhimu. Uwepo wa Messi
uwanjani ulitosha kuifufua timu yake na katika hilo hakuna kocha wa timu
pinzani ambaye ameweza kujua mbinu ya kuzuia hilo.
Inavutia
Kwenye timu ya taifa ya Argentina, Messi amefunga mabao 32
kwenye mechi 79. Rekodi yake ya kufunga huku haiendani na rekodi yake akiwa na Barcelona,
lakini hilo linaweza kutetewa na ukweli kuhusu soka la kimataifa.
Tofauti na Barcelona, wachezaji ambao wanatengeneza timu ya
taifa ya Argentina wanakutana mara chache sana. Hawajazoea kucheza pamoja kama
ilivyo kwa Xavi na Andres Iniesta. Pia wakati Messi akiangalia zaidi
ushambuliaji wa Argentina, lakini timu hajajengwa kumtegemea yeye.
ya kumlinda iwe rahisi, Argentina
walicheza na Marekani Machi 2011, ilikuwa mechi ya kirafiki ilichezwa katika
Jiji la New Jersey.
Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 1-1, siku hiyo Messi hakufunga
bao, kipa wa Marekani, Tim Howard, anayecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya
Everton, aliita kujipanga kwa Messi uwanjani kama kunavutia sana kumuangalia.
Kuna makala moja, iliandikwa kuelezea staili ya soka ya Argentina
kwa wakati huo, staili ambayo inahusisha upigaji wa pasi fupi fupi za haraka na
kumtengenezea mpira wa mwisho Messi kutokea katikati. Lakini kama Messi hakuhusika
kwenye kumalizia shambulizi hilo, basi alikuwa kati ya uwanja akihusika kwenye
kuanzisha mashambulizi, kama ilivyo akiwa Barcelona.
Kuelezea hilo, Howard alisema Messi huonekana kama anayetaka
kupiga pasi siyo shuti: “Siku zote huwa najaribu kusoma miguu yake, na kuona
wapi pasi inaenda na kusoma wachezaji wengine wanaoweza kuleta madhara kutokana
na pasi zake.”
‘Mchawi’
Kwa kumalizia, kitu muhimu zaidi katika kumzuia Messi kwa
mujibu wa Howard, ni kutokuwa na papara wala kupaniki mkimuona, Messi anaweza
‘uchawi’ wake na kufunga kabla hata mabeki kujua nini kimetokea.
Lakini cha kutisha zaidi kwa mabeki ni kwamba Messi huwa
hasubiri mpaka mtu akosee ndio afunge. Kama ambavyo kiwango chake cha mwaka 2012
kilivyothibitisha kwamba mchawi huyo anaweza kuizuru beki ya timu yoyote muda
wowote.
Hata pale timu yake inapofungwa Messi hufanya jambo ambalo
huwaacha watu vinywa wazi.
Beki wa Chelsea, John Terry aliwahi kusema: “Kwangu mimi Messi
ni mchezaji bora wa muda wote, ni mtu poa sana, na ni heshima kwa mchezaji
kwangu mimi anakila kitu. Ni Mchawi.”
No comments:
Post a Comment