BOSI wa Manchester United, Sir Alex
Ferguson, anatarajia kustaafu mwishoni mwa msimu huu baada ya miaka 26 ya
mafanikio kuongoza timu hiyo ambayo inashiriki Ligi Kuu England.
Ulimwengu wa soka umemmiminia sifa Ferguson
wakisema alikuwa kocha bora ambaye ametokea kuishi duniani.
Ferguson mwenye umri wa miaka 71
alidhibitisha uamuzi wake Jumatano asubuhi kwamba safari yake ya kuifundisha
Manchester United itafika kikomo mwishoni mwa msimu huu.
Wachezaji wa zamani wa Manchester United
Paul Ince na David Beckham walisema kuwa Ferguson aliwafanya kama watoto wake.
PAUL INCE
“Nakumbuka siku ya kwanza nilipoenda
Manchester United, nilishindwa kufuzu vipimo vya afya na nikawaza kuwa mpango
wangu wa kujiunga na timu hiyo utakuwa umekufa,” alisema Ince. “Hata hivyo,
Ferguson alinihali kama motto wake.”
“Kucheza chini yake haikua rahisi.
Alikua mtu wa mahitaji mengi. Alikuwa na wakati mzuri na mbaya na wachezaji
wengi katika msimu 1992-93, lakini anastahili heshima. Alifanya niwe mchezaji
mzuri mwenye kiwango kikubwa.
“Nilipokua Blackburn kama kocha na mambo
yakawa hayaendi vizuri, tulicheza na Manchester United Uwanja wa Old Trafford
na nilitumia dakika 15 au 20 kwenye ofisi yake.
“Aliniambia: ‘Ushauri pekee ninaoweza
kukupa ni usiruhusu wachezaji wakufanye ‘katuni’. Usiwape chochote kwasababu,
ukiwapa hata kidogo, watachukua kubwa. Jinsi kiwango chako kinavozidi kupanda
unapaswa kuzidi kushikilia msimamo wa ujumbe huu’.”
DAVID BECKHAM
Beckham ambaye alishawahi kuicheza
Manchester United chini ya Sir Alex Ferguson alisema kocha huyo raia wa
Scotland alifanya mabadiliko makubwa na kuwa na mafanikio katika timu hiyo
labda kuliko kocha mwingine.
“Mchango ambao alikuwa nayo kwa timu,
wachezaji na mashabiki, sidhani kama kuna mtu mwingine kwenye ulimwengu wa soka
ambaye anaweza kuwa na mchango kama huo,kamwe!” alisema Beckham ambaye
anaichezea Paris Saint-Germain ya Ufaransa.
VINCENT KOMPANY
“Sir Alex, mmoja kati ya makocha bora wa
miaka yote. Baada ya miaka 26 ya mafanikio katika soka, wote tunapaswa
kumshukuru kwa mchango wake.”
MICHAEL OWEN
“Bado hainiingii! Manchester United bila
Sir Alex Ferguson sihisi ipo sawa. Alikuwa mwanamume haswa ni bora ameamua
mwenyewe”
KASPER SCHMEICHEL
“Ni zaidi ya kuvunjika moyo! Meneja bora
ambaye amewahi kuishi! Hakuna swali!”
DANNY SIMPSON
“Wow siamini kama Sir Alex amestaafu.
Haionekani kama ni kweli. Yeye ni shujaa na ninaona faraja kusema kwamba
nimefanya naye kazi”
ROMELU LUKAKU
“Inasikitisha kuskia kwamba mmoja kati
ya mameneja bora amestaafu. Sir Alex alikuwa bingwa wa kweli na shujaa.”
CHELSEA FC
Sisi wote katika Klabu ya Chelsea
tunapenda kumtakia Sir Alex Ferguson kila la heri anapostaafu. Amekua mpinzani
mzuri kwa miaka 26.”
NEIL LENNON
“Soka haitakuwa kama tulivyozoea bila
Sir Alex…ameleta mchango mkubwa sana katika mchezo wa soka… sidhani kama kuna
mtu anaweza kumbadili.”
PETER SCHMEICHEL
“Nimesikitishwa, nimeshtuka,
nimehuzunika. Sikudhani kama kama hiyo siku itakua leo.”
SEPP BLATTER
“Nimetoka kuskia kwamba Sir Alex
Ferguson anastaafu mwishoni mwa msimu huu. Mafanikio yake kwenye soka
yanamfanya awe bila pingamizi meneja bora.”
GIUSEPPE ROSSI
“Kazi nzuri! Najivunia kuwahi
kufundishwa na Sir Alex Ferguson.”
CRISTIANO RONALDO
“Asante kwa kila kitu bosi.”
No comments:
Post a Comment