Timu Sita zafuzu Fainali za AFCON 2027
Baada ya kukamilika kwa raundi ya nne ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), timu sita zimefanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali hizo.
Timu zilizofuzu
rasmi ni pamoja na Morocco, Benin, Burkina Faso, Cameroon, Senegal na Mali,
ambazo zinaungana na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda zilizokwisha fuzu mapema
kwa kanuni ya kuwa wenyeji wa mashindano hayo.
Morocco
iliendeleza ubabe wake katika Kundi A kwa kuifunga Niger bao 1-0 na kufikisha
pointi 12 kileleni, ikiziacha Gabon, Niger na Lesotho zikigombea nafasi moja
iliyobaki.
Katika Kundi F,
Burkina Faso ilipata ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Mauritania na
kufikisha pointi 10, matokeo yaliyoiwezesha kufuzu pamoja na Benin zenye pointi
sawa na kuacha timu za Mauritania na Afrika ya Kati zikibaki nyuma.
Katika
mechi zingine, Mali ilijihakikishia nafasi ya kufuzu kwenye Kundi K baada ya
kuichapa Rwanda mabao 2-0 jijini Kigali na kufikisha pointi 10. Ushindi wa
Comoro wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Congo Brazzaville uliifanya Cameroon pia
kukata tiketi ya AFCON 2027.
Wakati huo huo,
Uganda ilitoka sare ya 1-1 na Botswana jijini Gaborone na kuendelea kuongoza
Kundi H ikiwa na pointi sita, huku ikijiandaa na fainali hizo ambapo tayari ina
tiketi ya uenyeji mkononi.
Post a Comment