Rais Samia na Rais Museveni Wazindua Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Mpigi Uganda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, wamezindua rasmi Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo eneo la Mpigi nchini Uganda.
Uzinduzi huo umefanyika tarehe 19 Novemba 2026 ambapo viongozi hao wawili waliongozana katika tukio hilo muhimu linaloashiria kuimarika kwa ushirikiano wa kiuchumi na viwanda kati ya nchi hizo mbili za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mara baada ya kuwasili katika eneo la kiwanda hicho kilichopo Mpigi, Rais Samia alilakiwa na mwenyeji wake Rais Museveni ambapo walipata fursa ya kusalimiana na kufanya mazungumzo mafupi kabla ya kuendelea na ratiba kuu ya uzinduzi. Viongozi hao wawili walikata utepe kwa pamoja kama ishara rasmi ya kukizindua kiwanda hicho cha magari.
Baada ya ufunguzi huo, Marais hao walifanya ziara ya kukagua kiwanda cha Double Q Automotive Assembly Plant kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji, teknolojia inayotumika na hatua zinazofuatwa katika kuunganisha magari nchini humo. Hatua hii inaelezwa kuwa chachu kubwa ya kukuza sekta ya viwanda, kutoa fursa za ajira kwa vijana na kukuza biashara ya kikanda ndani ya Afrika Mashariki.


.jpeg)


.jpeg)



Post a Comment