Jukwaa la Tanzania Fashion Forum 2026 Kukutanisha Wadau wa Mtindo na Biashara
Wabunifu wa mavazi, mafundi, wazalishaji wa nguo, wafadhili wa fedha,
wanunuzi pamoja na wataalamu wa sekta ya utalii wanatarajiwa kukutana katika
ukumbi wa Little Theatre jijini Dar es Salaam tarehe 24 Novemba 2026.
Mkutano huo unaojulikana kama Tanzania Fashion Forum 2026 ni sehemu ya
msimu wa 19 wa Swahili Fashion Week & Awards na unalenga kufungua fursa
mpya za kibiashara kwa wadau wa sekta ya mitindo.
Jukwaa hili litafanyika kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana
chini ya kaulimbiu isemayo "Kujenga Uchumi wa Mitindo Tanzania — Kutoka
Ubunifu Hadi Biashara".
Katika kongamano hilo, mada mbalimbali muhimu zitajadiliwa ili kusaidia
kukuza biashara za mitindo nchini.
Wadau watapata nafasi ya kujadili jinsi ya kupata malighafi ya vitambaa
na washirika wa uzalishaji wa ndani, pamoja na njia za kupata ufadhili wa
kifedha.
Pia kutakuwa na majadiliano juu ya jinsi ya kubadilisha urithi wa
kisanii kuwa bidhaa za kisasa za kibiashara, mikakati ya kukuza mauzo kutoka
jukwaani hadi kwenye maduka ya jumla na rejareja, pamoja na jinsi sekta ya
mitindo inavyoweza kushirikiana na sekta za utalii na biashara kufikia wateja
wapya.
Tukio hilo limeelezwa kuwa fursa ya kipekee kwa yeyote anayejenga nembo
ya mavazi, anayejishughulisha na nguo, wanunuzi wa maduka, wawekezaji au
wanafunzi wa mitindo kupata majibu ya changamoto zao na kujenga mtandao wa kibiashara.
Kushiriki katika jukwaa hilo ni bure na liko wazi kwa umma, lakini
inalazimu kujisajili mapema kabla ya kuhudhuria.
Kwa maelezo zaidi na taratibu za usajili au tiketi za maonyesho, wadau
wanaweza kuwasiliana kupitia nambari +255 795 99 66 89 au +255 769 69 66 33,
barua pepe info@swahilifashionweek.com, au kutembelea tovuti ya www.swahilifashionweek.com
na programu za PIKI na Nilipe.

Post a Comment