Rais Samia Amteua Dkt. Evaline Munisi wa NCCR-Mageuzi Kuwa Naibu Waziri
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo katika safu ya uongozi kwa kumteua Mhe. Dkt. Evaline Wilbard Munisi (Mb.) kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano).
Dkt. Munisi, ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa kutokea chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi, anachukua nafasi ya Mhe. Rahma Riyadh Kisuo (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Katika hatua nyingine, mabadiliko hayo yaliyotangazwa leo tarehe 02 Mei, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, yamehusisha pia uhamisho wa Makatibu Wakuu.
Katika uhamisho huo Bw. Eliakim Chacha Maswi amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwenda kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum. Aidha, aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Antony Jingu, amehamishwa kwenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Maswi katika Wizara ya Katiba na Sheria.

Post a Comment