Samatta mchezaji bora wa mwezi Aprili 2026 Le Havre AC

 


Nyota wa Tanzania, Mbwana Samatta, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili 2026 katika klabu yake ya Le Havre AC inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1.

Katika mwezi huo, Samatta alifunga mabao mawili yaliyosaidia kuimarisha kiwango chake ndani ya timu hiyo.

Alifunga bao lake la kwanza Aprili 12, 2026, katika mchezo wa Ligue 1 uliomalizika kwa sare ya 1-1, likiwa ni bao lake la kwanza tangu ajiunge na Le Havre.

Bao lake lingine alifunga katika mchezo dhidi ya FC Metz, akitikisa nyavu dakika ya tano katika mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 4-4.

Kwa mafanikio hayo, Samatta ameendelea kuweka historia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kufunga mabao katika ligi kuu mbili kubwa barani Ulaya ambazo ni English Premier League alipokuwa na Aston Villa na sasa Ligue 1 akiwa na Le Havre.

No comments