HASHIM KAMBI AFARIKI DUNIA
Mwigizaji mkongwe wa filamu nchini Tanzania, Hashim Kambi, amefariki dunia leo.
Taarifa zinasema kwamba amefariki akipatiwa matibabu hospitali ya Mico Sinza.
Akizungumza na BSKY Media, Katibu Mtendaji wa wa Bodi ya Filamu Dk Gervas Kasiga amesema kwamba Hashim alikumbwa na shida wakati akirekodi na kukimbizwa hospitalini hapo.
Dkl Kasiga alisema kwamba alikuwa anaelekea hospitalini hapo .
Taarifa zaidi zinatarajiwa kutolewa baada ya taratibu za awali kukamilika.

Post a Comment