DK HOSEA AMPONGEZA SAMIA TUME YA UCHUNGUZI WA VURUGU




Rais Mstaafu wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Dkt.Edward Hosea, amesema anapongeza hatua ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuunda tume ya Uchunguzi ya matukio ya Oktoba 29,2025.

Dkt.Hossea amesema hayo Mkoani Iringa mapema leo wakati akizungumza na wanahabari na kueleza  kuwa uwepo wa tume hiyo kumesaidia kufanya watanzania kutulia na kusubiri mapendekezo ya tume yatalenga nini hasa na kusisitiza watanzania wana matumaini na tume hii.

“Naipongeza hatua ya Mh.Rais  ya kuunda tume,fikiria tusingekuwa na tume hali ingekuwaje?Kuwepo kwa tume hii kumesaidia kuwafanya watanzania watulizane wawe na matarajio kuona tume hii inapendekeza nini,kwa hivyo mimi naamini kabisa tume hii watanzania wana matumaini makubwa sana”.Alisema Dkt.Hossea.

Dkt.Hossea ameongeza kuwa Pamoja na yote yaliyotokea ataendelea kuwa muumini wa Tanzania kutafuta suluhu zake yenyewe hata kama taasisi za kimataifa zitakuja Tanzania na kutaka kujua kilichotokea.

No comments