Yassine Bounou Anyakua Tuzo ya Glovu ya Dhahabu AFCON 2025



Mlinda mlango bora wa sasa wa CAF, Yassine Bounou, ametunukiwa tuzo ya Glovu ya Dhahabu (Golden Glove) kama kipa bora wa mashindano ya TotalEnergies CAF Africa Cup of Nations 2025, akihitimisha mashindano hayo kwa kiwango bora cha binafsi langoni mwa "Simba wa Atlas".

Bounou alikuwa kama ukuta usiopenyeka katika mashindano yote, akifanikiwa kucheza mechi tano bila kuruhusu bao (clean sheets) kati ya mechi saba, rekodi inayomfanya kulingana na kipa wa Senegal, Edouard Mendy. Uimara wake ulisaidia Morocco kuruhusu mabao mawili pekee katika safari yao ya kuelekea fainali — jambo linalodhihirisha utulivu na ushawishi wake mkubwa kwa taifa hilo mwenyeji.

Katika mashindano yote, mkongwe huyo alifanya mfululizo wa sevu (saves) za hatari ambazo mara nyingi ziliipa Morocco faida. Moja ya nyakati zake bora ni pamoja na kuokoa michomo mikali kwenye hatua za mtoano na kiwango bora alichoonyesha nusu fainali, ambapo juhudi zake zilikuwa nguzo muhimu ya kuwavusha "Simba wa Atlas" hadi hatua ya fainali.

Licha ya Morocco kupoteza kwa uchungu bao 1–0 dhidi ya Senegal baada ya muda wa ziada, uwezo wa Bounou uwanjani ulimfanya astahili heshima hiyo.

Tuzo hii ya Glovu ya Dhahabu inaongeza sifa katika rekodi zake motomoto na kudhibitisha hadhi yake kama Kipa Bora wa Mwaka wa CAF, huku ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika safari ya Morocco kwenye michuano hiyo ya AFCON 2025.

No comments