Brahim Díaz Anyakua Kiatu cha Dhahabu (Puma Golden Boot) AFCON 2025
Nyota wa mashambulizi wa Morocco, Brahim Díaz, ametawazwa kuwa mshindi wa kiatu cha dhahabu cha Puma Golden Boot katika michuano ya TotalEnergies CAF Africa Cup of Nations 2025, kufuatia mfululizo wa mabao yaliyomweka kileleni mwa soka la Afrika.
Akicheza mbele ya mashabiki wa nyumbani wenye mapenzi ya dhati, fowadi huyo wa "Simba wa Atlas" alihitimisha michuano hiyo akiwa mfungaji bora. Mafanikio haya yanakuja baada ya kuibuka mfungaji bora pia katika hatua ya kufuzu AFCON 2025—rekodi adimu inayodhihirisha kiwango chake bora na umuhimu wake ndani ya timu ya taifa.
Díaz amemaliza michuano hiyo akiwa na jumla ya mabao matano. Licha ya Morocco kupoteza fainali, hakuna mchezaji mwingine aliyeweza kufikia idadi hiyo ya mabao, jambo lililomfanya staa huyo wa Real Madrid kuondoka na tuzo hiyo mikononi mwake.
Safari ya Mabao ya Díaz
Safari ya Díaz katika AFCON 2025 ilitawaliwa na umakini mkubwa langoni, akifunga mabao katika kila hatua muhimu ya Morocco:
Hatua ya Makundi: Alifunga bao la ufunguzi katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Comoro, kisha akafunga bao lingine katika sare ya 1-1 dhidi ya Mali.
Mvua ya Mabao: Alipiga "brace" (mabao mawili) dhidi ya Zambia na kuhakikisha ushindi mnono katika hatua ya makundi.
Hatua za Mtoano: Aliendeleza makali yake kwa kuifunga Tanzania katika hatua ya 16 bora, na kisha kuifunga Cameroon katika hatua ya robo fainali.
Kwa kufunga katika mechi tano tofauti, Díaz amejiunga na orodha ya wachezaji mashuhuri katika historia ya AFCON waliocheka na nyavu katika mfululizo wa michezo kwenye mashindano mamoja.
Historia Mpya Morocco
Kupitia ushindi huu wa Puma Golden Boot, Díaz ameingia rasmi kwenye vitabu vya historia vya soka la Morocco. Amekuwa mmoja wa wachezaji hatari zaidi wa Morocco kuwahi kutokea katika mashindano ya AFCON, huku akiweka kigezo kipya cha ufungaji bora kwa kufumania nyavu mfululizo kwenye fainali hizo.

Post a Comment