FIFA YATANGAZA DESEMBA 15 TAREHE YA MWISHO VILABU KUACHIA WACHEZAJI KWA AFCON 2025




Ifikapo Jumatatu, Desemba 15, 2025, vilabu vyote lazima viwe vimewaachia wachezaji wao kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco.

Fifa imesema kwamba  baada ya majadiliano yenye manufaa na wadau wa soka na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) imeona kipindi hicho ni muafaka kwa kuhakikisha kwamba hakuna upande unapata changamoto.

Kipindi cha kuachia wachezaji kimefupishwa kwa siku saba, ikiigwa mfumo uliotumiwa Kombe la Dunia la 2022, na hivyo kuhakikisha kwamba athari kwa vilabu vinavyoshiriki katika ratiba ngumu za ligi.

FIFA pia imehimiza Mashirikisho ya Wanachama na vilabu kufanya mazungumzo ya pande mbili kwa nia njema ili kutafuta mwafaka kwa wachezaji wanaohusika katika mashindano ya mabara.

Pale ambapo mizozo itaendelea, FIFA itapatanisha, kwa kutumia miongozo inayolingana na kila changamoto, ikiwa ni pamoja na ratiba za mashindano, hatua ya mashindano husika, na ushiriki wa mchezaji kihistoria na unaotarajiwa.

Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 litafanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21, 2025, hadi Januari 18, 2026.

No comments