SAIBARI AMLIZA MAMA YAKE KOMBE LA DUNIA
Ismael Saibari (25) na
historia yake ya kukatisha tamaa.
Katika umri wa miaka miwili, nyota huyo wa timu ya
taifa ya Morocco alipata athari za miguu kutokana na ugonjwa ambao ulimsumbua tangu
kuzaliwa kwake.
Madaktari waliwaambia wazazi wake kwamba ni ngumu
kwa mtoto wao kuja kutembea vizuri kama ilivyo kwa binadamu wa kawaida.
Baada ya mwaka mmoja wa matibabu kwa kutumia vyuma maalum vya kusaidia miguu , utembeaji wa Saibari ulianza kuimarika na lengo pekee la mama yake lilikuwa ni kuona mwanae anatembea na kuishi maisha ya kawaida.
Baadaye, alipokuwa na umri wa miaka 7, familia yake ilihamia Ubelgiji.
Baadaye alifichua kwamba alienda kufanya majaribio katika klabu ya Anderlecht lakini akakataliwa kwa "kuwa mzito." Hata hivyo, Mechelen na Genk walimkubali katika akademi zao, ambako aliendeleza mchezo wake hadi kujiunga na PSV mwaka 2020.
Sasa amefikisha umri wa miaka 25, Saibari ameibuka
kuwa mmoja wa nyota muhimu na tegemeo katika Kombe la Dunia la 2026 akiwa na
Taifa lake.
Licha ya changamoto kubwa alizopitia ikiwemo
kuachwa na akademi yake akiwa na umri wa miaka 14 kwa sababu ya kuwa na uzito
mkubwa uliopitiliza lakini hakukata tamaa.
Machozi ya mama yake yamemwagika leo kwa furaha
baada ya kukumbuka mapito ya mtoto wake ambaye ni fahari ya Morocco kwasasa.

.jpg)
Post a Comment