Serikali yaipa neno Twiga Stars Wafcon Morocco



Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ameitaka timu ya soka ya taifa ya wanawake, 'Twiga Stars' kuhakikisha inafanya vizuri kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (WAFCON) zitakazofanyika Morocco mwakani.

Msigwa alisema hayo kwenye hafla maalamu ya kuipongeza Twiga Stars kufuzu fainali hizo ambapo pia alikabidhi Sh milioni 50 kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa benchi la ufundi na wachezaji wa timu hiyo.

"Fedha hizi zimetolewa na Rais Samia kwa kutambua utendaji wenu mzuri. Mmepeperusha bendera ya taifa tunajisikia. Msibweteke na zawadi hizi, bali ziwe chachu ya kufanya vizuri zaidi WAFCON," alisema Msigwa.

Aliwapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kujiituma, jambo ambalo lililoweka Tanzania kwenye ramani ya soka Afrika.

Msigwa alibainisha kuwa timu za wanawake zimekuwa na maono ya kutupa, kwani zimekuwa zikifanya vyema katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.

Aliahakikishia kuwa serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), itaendelea kuiunga mkono Twiga Stars ili iendelee kufanya vizuri zaidi.


No comments