BREAKING NEWS: Hali ni Shwari, picha zinazotembea ni za nyuma




 Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa taarifa kwa umma, likiwaonya Watanzania kuhusu mbinu zinazotumiwa na wachochezi wa mitandaoni, ambao wanatumia picha na video za zamani zinazopotosha kuhamasisha vurugu.

Msemaji wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi jijini Dodoma, ameeleza kuwa hadi muda huu wa mchana tarehe 9/12/2025, hali ya usalama nchini ni shwari.

Jeshi la Polisi llimetoa wito kwa wananchi waendelee kuzipuuza picha, mijongeo na minato zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa kuna maandamano yameanza.

Taarifa hizo za uchochezi zinalenga matukio ya zamani:Baadhi ya picha na video zinazotumiwa zinahusu matukio ya tarehe 29, 30, na 31 Oktoba 2025.

Nyingine zinarudi nyuma zaidi, mfano, matukio ya mwezi Juni 2025 ambapo kabila la Wamaasai walikuwa wakisherehekea jando walizofanyia msitu wa TANAPA Jijini Arusha.

Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuimarisha ulinzi na usalama nchini, huku vikilinda maisha ya watu na mali zao.


Uhalali wa Maandamano

Polisi imekumbusha kwamba maandamano yanayopewa jina la 'maandamano ya amani' yaliyopigwa marufuku tangu tarehe 5 Disemba 2025 yanakiuka matakwa ya kisheria.Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi waendelee kufuata sheria kwa manufaa ya Watanzania wote.


No comments