Kocha Mkuu
wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes Ammy Ninje
ameahidi ushindi katika mchezo wao wa raundi ya pili kufuzu fainali za Africa
za Vijana dhidi ya Mali utakaochezwa Jumapili Mei 13, 2018 kwenye Uwanja wa
Taifa.
Ninje alisema Mali ni timu nzuri ambayo amekuwa akiifuatilia
kwa karibu lakini kwa upande wao wamekuwa katika maandalizi ya kuhakikisha
wanafanya vizuri na wachezaji wanaonekana kuyashika vyema mafunzo yake.
Amesema hata kambi ya kikosi hicho imekuwa na morali kubwa
yenye kiu ya kutaka kufanya vizuri na kufuzu kwenda raundi ya Tatu ambayo ndio
ya mwisho kabla ya kufuzu kucheza fainali hizo za Africa kwa vijana.
Amewataka waTanzania kujitokeza kwa wingi Jumapili ili
kuwaongezea nguvu zaidi vijana hao ya kufanya kile ambacho wa
Tanzania wengi wangependa kukiona.
Naye Issa Makamba nahodha wa kikosi hicho amesema wachezaji
wako tayari kwa mapambano ambayo wanaamini watashinda.
Katika mchezo huo utakaoanza saa 10 jioni Kiingilio kwa VIP
zote shilingi 3,000 na Mzunguko shilingi 1,000.
No comments:
Post a Comment