SHIRIKISHO
la Soka Barani Afrika (CAF) limeteua waamuzi wanne kutoka nchini Angola
kuchezesha mchezo wa kombe la shirikisho hatua ya makundi kati ya Yanga na
Rayon unaotarajiwa kuchezwa Mei 16 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo
ambao utaanza saa 1:00 usiku utachezeshwa na mwamuzi ni Helder Martins
Rodrigues akisaidiwa na Ivanildo Meirelles De O Sanche na Wilson Valdmiro
Ntyamba na mezani atakuwepo Joao Amado
Muanda, kamishna atakuwa Abebe Solomon Gibresilassie kutoka Ethiopia.
Awali mchezo
huo ulikuwa uchezeshwe na waamuzi kutoka Kenya lakini wambedalishwa kutokana na
timu ya Gor Mahia kuwa kundi moja na Yanga na Rayon pamoja na USMA Algier.
Yanga
itakutana na Rayon ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa USMA
Algier wakati Rayon walitoka sare na Gor Mahia.
Wakati huo
huo TFF imeitaka Yanga pamoja na AFC ya Arusha
na Coastal Union ya Tanga kufanya uchaguzi kujaza nafasi za viongozi wake
waliojiuzulu
Yanga imekuwa chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti, Yussuf Manji Mei mwaka jana.
Manji aliingia Yanga mwaka 2006 kama mdhamini kupitia kampuni yake ya
Lotto Kitita, lakini baadaye akawa mfadhili Mkuu wa klabu kabla ya kuwa Mwenyekiti.Yanga imekuwa chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti, Yussuf Manji Mei mwaka jana.
No comments:
Post a Comment