KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Mipira wa Miguu (TFF) imemfungia
mechi tatu na kumpiga faini ya Sh. 500,000 beki wa Mbeya City, Ramadhani Malima
kwa kitendo cha kuingia uwanjani kushangilia bao baada ya kutolewa kwa kadi
nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City April 22
kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Ofisa habari wa TFF, Cliford
Ndimbo alisema kamati hiyo ilikutana Mei 9 na kusikiliza mashauri manne tu huku
kocha wa Azam Ciaoba na beki wa Yanga Kelvin Yondani wakishindwa kufika katika
kamati hiyo bila taarifa
“Ramadhani Malima alitolewa kwa
kadi nyekundu lakini baada ya timu yake kusawazisha bao mchezaji huyo
alionekana uwanjani akishangilia na wachezaji wengine,”
“Kutokana na kosa hilo Malima amefungiwa mechi tatu ambayo mechi moja
ameshaitumikia hivyo zimebaki mechi mbili na faini ya kiasi cha Sh. 500,000
"alisema Ndimbo.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Shomari Lawi wa Kigoma akisaidiwa na Omar Juma wa Dodoma na Godfrey Kihwili wa Arusha, Yanga ilitangulia kufunga bao kipindi chake cha kwanza lililofungwa na Raphael Daudi kabla ya Mbeya City kusawazisha kipindi cha pili kupitia kwa Iddi Suleiman Nado.
Malima alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 65 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kumfuatia kumchezea rafu kiungo wa Yanga, Yussuf Mhilu, lakini akarejea uwanjani kushangilia bao la kusawazisha la timu yake katika dakika za mwishoni.

Pia kamati hiyo imewafungia kucheza mechi tatu na faini ya Sh. 300,000
kila mmoja kutokana na kwa kitendo cha kutaka kumpiga mwamuzi katika mchezo wa
Ligi daraja la pili dhidi ya Namungo FC
Naye Katibu wa Mlandizi Queens, Rukia Michael amefungiwa miezi miwili na
kutozwa faini ya Sh. 200,000 kwa kosa la kutaka kumpiga mwamuzi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake dhidi
ya timu yake na Kigoma Sisters uliochezwa kwenye Uwanja wa Mabatini Pwani.
Mashauri
mengine kadhaa hayakusikilizwa baada ya kutofika kwa washtakiwa wa mashauri
hayo na kamati imeomba wapewe wito wa mwisho ambao kama hawatafika kamati
itasikiliza mashauri yao katika upande mmoja na kuyatolea maamuzi.
Ambao
hawakufika na hawakutoa taarifa ni George Rast na Shaibu
Salim(AFC-Wachezaji),Aristica Cioaba(Azam FC-Kocha),Issa Ngwasho(JKT
Mlale-Meneja),Hosea John,Rashid Ally,Hamis Athuman,Casmir Focus(JKT
Msange-Wachezaji),Joseph Mkota(JKT Oljoro-Mchezaji),Katregea Kalegea(Mashujaa
FC-Mchezaji),Cuthbet Japhet(Toto Africans-Afisa habari),Kelvin Yondan(Young
Africans-Mchezaji) wakati Meneja wa Singida United Ibrahim Mohamed yeye alitoa
taarifa ya kufiwa na baba yake mzazi.
No comments:
Post a Comment