JOHN Bocco na Emmanuel Okwi leo wameipatia Simba ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Prisons katika mechi ya Ligi Kuu
iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya
Simba izidi kujisafishia njia kuelekea kwenye ubingwa kwani sasa inaongoza msimamo
wa ligi ikiwa na pointi 58 juu ya mabingwa watetezi Yanga walio na pointi 47 na
mechi mbili kibindoni.
Mabao ya Simba
yalifungwa katika kila kipindi kwenye mechi hiyo hiyo ambayo vinara hao
walitawala katika vipindi vyote.
Prisons ilionekana
kuibana Simba katika dakika za mwanzo kabla ya kusalimu amri na kuruhusu bao la
Bocco dakika ya 35 kabla ya kujikuta wakicheza mchezo wa kujilinda zaidi katika
kipindi cha pili.
Bocco alifunga bao
hilo la kuongoza kwa kuuwahi kwa kichwa mpira wa krosi wa Erasto Nyoni
uliogonga mwamba kabla ya kuujaza wavuni.
Okwi aliifungia Simba
bao la pili katika dakika ya 80 na kuendelea kukifukuzia kiatu cha dhahabu kwa
kufikisha mabao 18 kwenye ligi.
Penalti ya Okwi
ilitolewa na mwamuzi Shomari Lawi wa Kigoma baada ya Jumanne Elifadhili
kumfanyia madhambi Bocco akiwa kwenye eneo la hatari, Elifadhili alioneshwa
kadi nyekundu.
Katika mechi hiyo
Simba ilikosa mabao mengi hasa kupitia kwa mchezaji wake Shizza Kichuya
aliyekosa mabao dakika ya kwanza, 50, 62 na 70.
Mechi nyingine zilizochezwa Ndanda ikiwa nyumbani Nang'wanda Sijaona imeshindwa kutamba kwa kukubali ‘kupapaswa’
na Ruvu Shootinga mabao 3-1 huku Kagera Sugar ikishinda 2-1 dhidi ya ndugu zake
Mtibwa Sugar kwenye uwanja wake wa nyumbani Kaitaba.
No comments:
Post a Comment