RAIS Magufuli na waigizaji wa
filamu Yvonne Cherrie 'Monalisa' na Ray Kigosi wameibuka washindi
kwenye tuzo za kifahari za Afrika 'The African Prestigious Awards' nchini Ghana
Katika tuzo
hizo zilizotolewa juzi Accra nchini Ghana, Monalisa ametwaa tuzo katika
kipengele cha mwigizaji bora barani Afrika na kumbwaga mpinzani wake Lupita
Nyong'o.
Ray Kigosi ameshinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume barani Afrika
na Moiz Hussein alishinda katika kipengele cha mpigapicha bora
Monalisa alithibitisha
ushindi huo kupitia mtandao wake wa Instagram akiwa na picha ya tuzo yake na
kuandika, “Tumeshindaaaaaaa narudi nyumbani na tuzo za kutosha, ahsante
Watanzania, nawapenda mno,”.
Kwa ujumbe
huo wa Monalisa ina maana huenda pia kuna tuzo nyingine Watanzania ambazo
wameshinda kwani walikuwa wanawania
vipengele mbalimbali katika tuzo.
Watanzania
wengine waliokuwa wanawania ni King Majuto kipengele cha mchekeshaji bora
Afrika, Vicent Kigosi kipengele cha msanii bora wa kiume Afrika na mpigapicha mahiri
ambapo alikuwepo Moiz Hussein
Monalisa
kabla ya kuondoka alikatiwa tiketi ya ndege na kuagwa na Waziri wa Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.
No comments:
Post a Comment