MWIGIZAJI Yvonne
Cherrie 'Monalisa’ ambaye
amepata tuzo ya mwigizaji bora Afrika zinazotolewa na The African Prestigious Awards' nchini Ghana juzi anatarajiwa kuipeleka tuzo hiyo
bungeni ikiwa ni nembo ya ushindi wa taifa.
Katika tuzo
hizo mwizagizaji Ray Kigosi aliibuka mwigizaji bora wa kiume na mpigapicha
mahiri alikuwa Moiz Hussein wa Tanzania pia huku Rais Dk John Pombe Magufuli akaipata kwa upande wa viongozi bora Afrika.
Akizungumza
jana mama mzazi wa Monalisa anayeitwa Natasha Lewis alisema baada ya Monalisa kurudi kutoka
Accra Ghana anatarajiwa kwenda Dodoma kwa ajili ya kuipeleka tuzo hiyo bungeni.
Naye Monalisa
kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwashukuru Watanzania wote kwani ni zaidi
ya miaka 19 sasa akiwa kwenye sanaa na wamekuwa nyuma yake na tuzo aliyoipata
ni kwa ajili yao kwani bila mashabiki isingewezekana.
Wakati huo
huo Ray Kigosi amesema alishindwa kuhudhuria tuzo hizo kwa sababu alikuwa nje
kikazi
“Sikufanikiwa
kuhudhuria kwenye tuzo hizo kwa sababu nikuwa Afrika Kusini kikazi sina cha
kuwalipa ndugu zangu zaidi ya kuendelea kuwaletea kazi nzuri zenye viwango bora
ili tuendelee kuiletea heshima nchi yetu,” alisema Ray Kigosi
Tuzo
hizo zilizotolewa usiku wa kuamkia April 15, 2018 mjini Accra nchini Ghana, Ray
na Monalisa waliibuka washindi kutoka Tanzania.
No comments:
Post a Comment