MAKALA: HOTUBA YA RAIS SAMIA URUSI NI USHINDI KIUCHUMI, KIJAMII, NA KIDIPLOMASIA!
Na Beda
Msimbe,TBN, aliyekuwa Urusi
IJUMAA Juni 5,
2026 ilikuwa siku ya kihistoria na ya kipekee, wakati Rais wa Tanzania, Samia
Suluhu Hassan, alisipomama mbele ya viongozi wa dunia katika Jukwaa la
Kimataifa la Uchumi (St. Petersburg International Economic Forum) na hoja nzito
zenye mashiko, akibeba sauti ya Watanzania wote na kuweka wazi fursa
zinazopatyikana Tanzania ikiwa na pamoja na mwelekeo mpya wa nchi katika
kutengeneza uchumi wa kisasa.
Jukwaa hilo
lilikuwa sehemu muhimu ya ziara ya Rais Samia ambayo haikuwa tu ya itifaki,
bali ya kueleza milango wazi ya fursa za kiuchumi na kijamii.
Jinsi Rais
Samia alivyopokewa na kukirimiwa nchini Urusi katika shughuli zoye zilizomhusu,
ilionesha taswira ya urafiki wa dhati na cheko tupu kati yake na mwenyeji wake,
Rais Vladimir Putin. Ziara hiyo ilirudisha historia, ikaweka wazi haja ya sasa
baada ya ukombozi wa kisiasa kusaidiana kupatikana kwa ukombozi wa kiuchumi na
ustawi wa jamii zote mbili.
Akiwa katika jukwaa la kiuchumi, akizungumza na washiriki hotuba ya Rais Samia iliwatafakarisha wahusika, kwani ilkijaa hoja za uchambuzi wa kina na haja ya dunia kubadilika
Rais Samia
alifanya uchokozi wa fikira na moja ya uchokozi huo alisema bila kupepesa kuwa
ifikapo mwaka 2050, mtu mmoja kati ya wanne duniani atakuwa Mwafrika; na
takwimu hizo kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ziliambatana na swali:
"Je, Afrika itastawi na kukuaa kwa masharti ya nani, na kwa modeli ya nani
ya uchumi?"
Swali hilo
lenye mantiki kubwa liliulizwa kwa shauku kubwa kutokana na siasa za kijiopiti
ambazo zimekuwa zikiyumbisha ushirika wa kawaida na kujazwa na masharti ya
kuangushana na kudhibitiana katika mfumo ambao unamlazimisha maskini asiendelee
au kuchaguliwa patna wa kuzungumza naye.
Katika misingi
mikubwa ya kufikiri kilojiki Rais Samia alikuwa anaitafadhalisha dunia sio
kuistiri Afrika bali kutambua ukweli na kuiacha Afrika ijiamulie mambo yake
yenyewe.
Mathalani
Afrika kwa sasa ina Ajenda 2063 na soko la AfCFTA, lakini kuna mataifa
yanayoendelea kuingilia kati kila mara na kuwatenganisha waafrika ili
wajifikirie wanahitaji masaada katika utatuzi wa kero zinazowakabili.
Rais Putin
aliunga mkono hoja hiyo, jambo lililoleta miguno ya ridhaa na vigelegele
ukumbini.Kuna mambo mengi yanayopaswa kufanywa na Waafrika wenyewe yenye
manufaa makubwa kwa binadamu
Mambo
yaliyoguswa
Katika hotuba
yake na ziara hiyoik ya Urusi Rais Samia amegusa mambo mengi. Hapa tunaweza
kuangazia maeneo makubwa yaliyoguswa na jinsi makubaliano yalivyomalizika ikiwa
ni mafanikio makubwa kwa Tanzania.
Ikumbukwe
kwamba ndani ya ziara ya Rais Samia ambapo pia aliambatana na wafanyabiashara
inakumbusha ulimwengu kuhusu mizizi imara ya kidiplomasia kati ya Tanzania na
Urusi. Kuna historia ndefu ya mahusiano kuanzia miaka ya uhuru,kwani siku mbili
baada ya Tanzania bara kupata uhuru, Urusi ilituma salamu vivyo hivyo kwenye
mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Mbele ya
wawekezaji, Rais Samia alibainisha kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi ya
takribani 6%, ukiwa miongoni mwa chumi zinazochangamka zaidi Afrika.
Alitangaza Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kumfikisha kila Mtanzania kwenye kipato
cha wastani cha dola $7,000$ huku akielezea fursa za uwekezaji na biashara
nchini Tanzania
Hotuba yake
hiyo iliyopigiwa makofi mara kwa mara iliwavutia matajiri wa Kirusi, ambapo
sekta binafsi ya Urusi ilikiri kuwa Tanzania ni soko salama na lenye utulivu wa
kisiasa unaoruhusu ukuaji wa mitaji.
Lakini hayo
yamesemwa wakati pia Rais akieleza kuwapo kwa Mapinduzi makubwa ya Miundombinu
(Reli na Bandari). Rais Samia ambaye katika mkutano huo pamoja na ule wa
pembeni ambapo wafanyabiashara wa Tanzania walipata nafasi ya kuzungumza na
wenzao wa Urusi, alieleza kwa kina ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
inayounganisha Bandari ya Dar es Salaam na nchi za Rwanda, Burundi, na DRC na
faida yake kwa wakazi wa eneo hili.
Pia alitaja
mpango wa miaka mitano (2026–2031) wa kupanua reli hiyo hadi Musoma, na
kuunganisha ukanda wa kusini kuelekea Malawi na Msumbiji. Urusi ikiwa na uzoefu
mkubwa wa teknolojia ya reli na usafirishaji, ilionesha nia ya kutoa utaalamu
wa kihandisi na mitambo ili kuharakisha uunganishaji wa reli hizo za kikanda.
Suala la kuwepo
kwa maboresho ya uwekezaji na mifumo ya saa 24 kulileta msisimko mkubwa. Rais
alieleza jinsi uwekezaji ulivyopaa kutoka dola bilioni 3 (2021) hadi dola
bilioni 12 (2025) kutokana na mfumo wa usajili wa kampuni unaochukua hadi saa
24 tu. Ni kutokana na kutambulika kwa ukweli huu Taasisi za uwekezaji za
Tanzania (TIC) na zile za Urusi zilisaini mikataba ya ushirikiano. Hatua hii
ilifungwa kwa cheko na bashasha, kwani urasimu sasa umepigwa marufuku rasmi.
Aidha Miradi ya
Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo na Bandari ya Kimataifa ya Mizigo ya
Mangapwani (Zanzibar) ilipewa kipaumbele cha juu na makampuni makubwa ya Urusi
yanayohusika na masuala ya meli na usafirishaji wa baharini. Wao walikubali
kutuma timu za wataalamu nchini Tanzania kufanya upembuzi yakinifu wa namna ya
kuwekeza kwenye bandari hizo.
Kwenye Sekta ya
Madini Rais Samia alizungumzia haja ya Tanzania ambayo ni Kuongeza Thamani
Ndani ya Nchi.Tanzania ikiwa na utajiri wa dhahabu, uranium, nickel, graphite,
helium, na madini adimu.
"Hatutaki
tena kuuza malighafi pekee, tunataka viwanda vya usindikaji hapa
nchini."alisema Rais Samia. Urusi, ikiwa ni mbabe wa madini, ilimalizia
haja ya Tanzania kwa kukubali kujenga viwanda (Industrial Parks) nchini
Tanzania ili kuchenjua na kuongeza thamani ya madini kabla hayajasafirishwa
kwenda nje.
Katikia ziara
hii Rais Samia alielezea na kudhihirisha ni kwa namna gani Tanzania iko tayari
kwa biashara, ubunifu, na ushirikiano wa kufanikisha kila hatua itakayochangia
ustawi wa wananchi wake.
Wakati Rais Samia akimaliza hotuba yake kwenye jukwaa hilo la St Petersburg kwa kutoa shukrani za dhati kwa Rais Vladimir Putin kwa ukarimu wake, viongozi hao wawili walionesha tabasamu la furaha, ikiwa ni ishara ya kukubalika kwa hoja za Tanzania na mwanzo mpya wa dhahabu katika uhusiano wa mataifa haya mawili.





Post a Comment