TANZANIA, UTURUKI KUSHIRIKIANA MAENEO 9 YA KIMKAKATI
Moja ya matunda ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Urusi ni kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika maeneo tisa ya kimkakati yatakayochochea ukuaji wa uchumi wa pande zote.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 7, 2026, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema Tanzania na Urusi zimeendelea kuwa marafiki wa muda mrefu, na ziara ya Rais Samia imefungua fursa mpya za ushirikiano katika sekta za kilimo, elimu na mafunzo, nishati, madini, viwanda, usafiri, utalii, uchumi wa kidijitali, biashara na uwekezaji.
Akizungumzia hatua za utekelezaji wa ushirikiano huo, Profesa Kitila amesema kuwa hadi sasa makubaliano kadhaa yamefikiwa.
Miongoni mwao ni mkataba wa ushirikiano kati ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Chuo Kikuu cha MGIMO, wa kuendeleza lugha ya Kiswahili nchini Urusi, huku lugha ya Kirusi ikitarajiwa kuanza kufundishwa nchini Tanzania.

Post a Comment