VIJANA WAHIMIZWA KULINZA AMANI YA NCHI

 


Mkuu Wilaya ya Ulanga,Khamana Juma Simba amewahimiza vijana wa Wilaya ya Ulanga kulinda amani ya taifa ili kila mmoja awe huru kufanya shughuli zake za maendeleo akisisitiza bila amani hakuna maendeleo.


 Simba ameyasema hayo katika uzinduzi wa Jukwaa la Vijana (Vijana Platform) ambalo lengo lake ni kuwakutanisha vijana wa makundi mbalimbali.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro, Salim Hashim amewaomba vijana kuchangamkia fulsa zinazopatikana katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga lakini pia ofisi yake imeandaa mpango maalumu wa kuwawezesha vijana kupitia mikopo isiyokuwa na riba ili kuwasaidia kuendeleza biashara zao.

No comments