KAGERA SUGAR YAREJEA LIGI KUU



Timu ya Kagera Sugar imefanikiwa kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao kufuatia ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya KenGold ya Mbeya katika mchezo wa raundi ya 28 ya Ligi ya Championship.

Ushindi huo umeifanya timu hiyo kufikisha pointi 68 ambazo haziwezi kufikiwa na mpinzani wake wa karibu, Polisi Tanzania, ambayo imepoteza mchezo wake dhidi ya Mbuni FC na kubakiwa na uwezo wa kufikisha pointi 66 pekee katika mechi mbili zilizosalia.

Katika msimu huu wa Championship, Kagera Sugar inayonolewa na Juma Kaseja imeonyesha kiwango thabiti ambapo katika mechi 28 zilizochezwa, imevuna ushindi katika mechi 21, ikipata sare tano na kukubali vipigo mara mbili pekee.

Baada ya kubadili makocha kadhaa Kagera Sugar ilishuka daraja msimu uliopita wa 2024/2025 ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Juma Kaseja ambaye ndiye kairejesha tena.


No comments