ZIARA YA RAIS SAMIA URUSI KULETA FAIDA NYINGI KWA WATANZANIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo ziara ya siku tatu ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Urusi itakwenda kunufaisha watanzania wa rika zote katika sekta mbalimbali za kimkakati ikiwemo elimu, utalii, kilimo na biashara.Akizungumza na Rais Samia akiwasili katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere ( JNIA), Balozi Kombo ameeleza kuwa ziara hiyo imegusa sekta zote muhimu huku akieleza kuwa ziara hiyo imefanyika wakati muafaka na imedhihirisha kuwa Tanzania ni rafiki wa mataifa yote na haina upande.
Ameongeza kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin amempa heshima kubwa Rais Samia Suluhu Hassa
ziara ya Rais Samia Urusi kuleta manufaa mengi kwa Watanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo, amesema ziara ya siku tatu ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Urusi itawanufaisha Watanzania wa rika zote kupitia fursa zitakazotokana na ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati, ikiwemo elimu, utalii, kilimo na biashara.
Akizungumza na TBC leo Juni 6, 2026 wakati Rais Samia akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Balozi Kombo amesema ziara hiyo imegusa sekta muhimu za maendeleo na imefanyika wakati mwafaka.
Ameongeza kuwa ziara hiyo imeonesha wazi kuwa Tanzania ni rafiki wa mataifa yote na inaendelea kufuata sera ya kutofungamana na upande wowote. Pia amesema Rais Vladimir Putin wa Urusi alimpa heshima kubwa Rais Samia, jambo lililoandika historia mpya katika mahusiano ya nchi hizo m

Post a Comment