Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 6, 2013

POINTI MOJA TU KUZISOGEZA TIMU ZA TAIFA ZA GHANA NA SENEGAL MBELE KUELEKEA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA.

Timu za taifa ya soka za Ghana na Senegal ni miongoni mwa timu tano ambazo zinahitaji alama moja mwishoni mwa juma hili kufuzu katika mzungunko wa mwisho wa kusaka tiketi yta kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil.

Mataifa saba yanatarajiwa kufuzu mwishoni mwa juma hili na kujiunga na Algeria, Misri na Cote Dvoire ambazo tayari zimeshafuzu kwenye timu kumi kabla ya kuchujwa na kupatikana timu tano wakilishi.

Cameroon, Ghana, Nigeria, Senegal na Tunisia zote zitakuwa nyumbani na zinahitaji sare ili kusonga mbele.

Kesho Ijumaa mchuano unasubiriwa ni kati ya Ghana na Zambia mchuano ambao wenyeji Ghana watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Baba Yaro mjini Kumasi.
Kikosi cha Ghana kikiongozwa na wachezaji kama Dede Ayew, Kevin-Prince Boateng na Michael Essien wanatarajiwa kuongoza kikosi cha Black Stars.


Kikosi cha Chipolopolo chini ya Kocha Harve Renard kinahitaji ushindi dhidi ya wenyeji wao ili kufuzu katika hatua ya mwisho lakini kikosi hicho kitakosa hudumu ya mshmabulizi Jacob Mulenga ambaye ana jeraha.

No comments:

Post a Comment