Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, September 4, 2013

DAKIKA 60 ZILIVYOTIKISA USAJILI LIGI KUU ENGLAND


LONDON, England

DIRISHA la usajili wa ligi mbalimbali ulimwenguni lilifungwa rasmi usiku wa kuamkia jana,  baada ya kila timu  kuhakikisha inawanasa nyota wanaoifaa.

Hata hivyo mchakato huo wa uliodumu kwa siku  64 ambazo ni sawa  na saa 1536  ulikuwa wa aina yake  katika Ligi Kuu ya England, ambapo ilishuhudiwa dakika 60 za mwisho wachezaji kama vile  Ozil, Fellaini, Coentrao na Lukaku wakitingisha usajili huo bada ya tetesi za musa wa  saa  11.

Mtikisiko huo wa kwenye ulimwengu wa dunia ulikuja siku ambayo tayari mvutano wa muda mrefu kuhusu usajili wa Gareth Bale, Luis Suarez, Wayne Rooney na Marouane Fellaini ukiwa umekamilika.
Hata hivyo, hadi saa 11:00 usiku kwa saa za Uingereza, kila kocha alikuwa bado akihaha kukamilisha usajili wake kabla ya dirisha hilo halijafungwa.

Katika dakika hizo  60 kuanzia saa  10.30 usiku hadi saa  11.30 ndipo iliposhuhudiwa kila kocha akipita kila kona ili kuhakikisha anainasa saini ya mchezaji aliyekuwa akimtaka.

Ufuatao ni muda ambao kila kocha alifanikiwa kuwa na uhakika na kile alichokuwa akikifukuzia kwa muda mrefu na hivyo kupumua.

1.Saa 10.30 usiku, muda huu ndiyo  Mesut Ozil alisaini kwenye fomu za kuitumikia  Arsenal

Katika muda huo kocha Arsene Wenger ndipo alipoutangazia umma wa mashabiki wa Arsenal kuwa amevunja rekodi ya klabu hiyo kwa kutoa pauni milioni 42.5 kumsainisha nyota huyo wa Real Madrid.

Katika mkataba huo, mchezaji huyo raia wa Ujerumani alisaini mkataba wa miaka minne na timu hiyo ya  Gunners, licha ya vinara wengine wa soka nchini Ufaransa, PSG  kutua mezani na ofa ya zaidi ya pauni milioni  140,000 kwa wiki ambazo nyota huyo atakuwa akilipwa kwenye klabu hiyo ya  Emirates.


1.11.06 usiku, Marouane Fellaini anamwaga wino kwenye mkataba wa  Manchester United
Katika muda huo ndipo ndoto za mchezaji Marouane Fellaini kuungana tena na kocha mpya wa Manchester United, David Moyes zilipotimia.
Katika makubaliano hayo, Everton na Man  United zilikubaliana kuuziana raia huyo wa Ubelgiji kwa pauni milioni 27.5.

3. Saa 11.18 usiku. Fabio Coentrao naye asaini mkataba na  Manchester United.

Inaelezwa kuwa muda huo ndipo nyota huyo aliyekuwa akiwindwa na kocha wa zamani wa timu hiyo, Alex Ferguson usajili wake ulipokamilika baada ya beki huyo wa kushoto wa timu ya Real Madrid, Coentrao alipowasili kwenye uwanja wa Old Trafford kwa mkopo wa muda mrefu.Hata hivyo inaelezwa kuwa hakuna siri kwamba Moyes alikuwa akimtaka beki wa kushoto wa timu ya Everton lakini hakuna shabiki wa Manchester United anaweza kulalamika kuhusu beki huo.

4. Saa 11.30... Romelu Lukaku anasaini  Everton.

Akiwa merejea Chelsea akitokea  West Brom ambako alikipiga kwa mkopo wa muda mrefu wengi walikuwa wakitarajia angekuwa chagu la kwanza kwenye safu ya ushambuliaji ya Jose Mourinho.

Hata hivyo kadri wiki zilivyokuwa zikienda, ilishuhudiwa Lukaku akitokea benchi mara tatu ambapo kati ya hizo, mojawapo ni  mechi ya ufunguzi wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, ambayo alikosa penalti dhidi ya Bayern Munich na kwa sasa amepelekwa  kwa mkopo wa muda mrefu kwenye klabu hiyo ya Goodison Park. Hatua hiyo inatafsiriwa kuwa huenda Mourinho amemuona Lukaku hafai kwenye kikosi kinachosaka ushindi na ndiyo maana akaamua kumpeleka huko.
Kwa kuondoka nyota huyo, Chelsea itakuwa imebaki na washambuliaji Fernando Torres na Demba Ba wakiwa chaguo la pili kwa nyota aliyenunuliwa msimu huu Samuel Eto’o.
Usajili zaidi uk.12&13

No comments:

Post a Comment