Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, April 30, 2013

HAPATOSHI USIKU HUU KATI YA REAL MADRID vs BORUSSIA DORTMUND UEFA CHAMPIONS LEAGUE


NDANI YA SANTIAGO BERNABEU, Nyumbani kwa Real Madrid, ndiko dimba la Mechi ya Marudiano ya Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONS LEAGUE, ambapo Real Madrid wataivaa Borussia Dortmund huku wageni hao wakiwa kifua mbele kwa ushindi wa Bao 4-1 toka Mechi ya kwanza iliyochezwa Wiki iliyopita.

Nusu Fainali nyingine itachezwa Jumatano pia Nchini Spain Uwanja wa Nou Camp ambapo Wenyeji Barcelona wanatafuta kupindua kipigo cha 4-0 walichowashwa na Bayern Munich Wiki iliyopita.
Wakati Real Madrid ya Jose Mourinho wakisaka Bao 3 kuitupa nje Borussia Dortmund iliyo chini ya Kocha Mkuu Jurgen Klopp, pia itabidi wasake dawa ya kumbana Straika hatari wa Dortmund, Robert Lewandowski kutoka Poland, ambae ndie alifunga Bao zote 4 Real walipotandikwa Bao 4-1 ndani ya Signal Iduna Park Jijini Dortmund.Kipa wa Real Hoi.. mechi ya kwanza, na zamu hii ataendelea kuwa hoi???...
Dortmund wakifanya mazoezi yao jana jioni Bernabeu tayari kumenyana naReal Madrid usiku huu wa leoTishio: Lewandowski (kushoto) naye akipasha hapa ..aliyewamiminia risasi zote Real MadridJogging: Marco Reus (left) and Mario Gotze (right) warm up at training Marco Reus (kushoto) na Mario Gotze (kulia) wakipasha jana jioniRATIBA:
MARUDIANO

Mechi kuanza Saa 3:45 Usiku

Jumanne Aprili 30
Real Madrid v Borussia Dortmund 1-4

Jumatano Mei 1
Barcelona v Bayern Munich 0-4
FAINALI
25 Mei 2013
UWANJA: WEMBLEY, London.

No comments:

Post a Comment