KIUNGO wa
klabu ya Tottenham Hotspurs Gareth Bale amekuwa mchezaji wa tatu kushinda tuzo
ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wakubwa na wachezaji wanaochipukia kwa
msimu mmoja
Tuzo hizo hutolewa
na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa nchini Uingereza. Mshambuliaji huyo wa
kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 23 ambaye pia alishinda tuzo ya wakubwa
mwaka 2011, amefunga mabao 19 katika ligi msimu huu na kuwa nyuma ya kinara wa
mabao Robin van Persie mwenye mabao 25 na Luis Suarez mwenye mabao 23.
Akikabidhiwa tuzo hiyo Bale amesema ni heshima
kubwa kwake kunyakuwa tuzo hizo mbili muhimu na kushukuru wapiga kura kwa
kutambua mchango wake haswa ikizingatiwa kumekuwa na majina makubwa mengine
katika orodha iliyokuwepo.
Bale
anaungana na wachezaji wengine walioshinda tuzo ya wakubwa mara mbili ambao ni
Cristiano Ronaldo, Thierry Henry, Alan Shearer and Mark Hughes wakati
walioshinda tuzo zote mbili kwa mwaka mmoja ni Ronaldo mwaka 2007 na Andy Gray
mwaka 1977.
No comments:
Post a Comment