Kocha huyo
wa Manchester United, wiki iliyopita aliweka wazi kuwa kuna uwezekano mkubwa
kwa Klabu yake kukataa kumuuza Mpoland huyo, hasa kutokana na Goetze kuwa
tayari kutua Bayern Munich kwa pauni milioni 32.
Fergie
alisema: “Mashabiki wa Dortmund hawatakuwa na furaha kuhusu Goetze na sidhani
kama watamuuza Lewandowski kwa Bayern Munich kwa sasa. Nina nafasi yake?
Ninaweza kutafuta nafasi kwa yeyote yule.”
@@@@@@@
@@@@@@@@
@@@@@@@
Ferguson: Scholes anaweza kustaafu
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex
Ferguson amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa Paul Scholes akatundika daluga
mwishoni mwa msimu. Scholes, 38, amekuwa akikabiliwa na majeraha mara kwa mara
msimu huu.
“Tutaona itakavyokuwa. Amekumbwa na
majeraha na yamekuwa yakimkera sana," alisema Ferguson. “Atakuwa hapa
mwaka ujao haijalishi ni mchezaji ama kocha.
“Utafika wakati ambao ni lazima aachie
ngazi, lakini bado anayo mengi yakutupa.”
Di Canio amtaka Suarez asiondoke
Liverpool
KOCHA wa Sunderland, Paolo di Canio
amemtaka Luis Suarez kuendelea kuitumikia Liverpool na kudhihirisha tabia yake
kwa wanaomkosoa.
Di Canio alisema: "Hawezi kunipiku
mimi, kwani nilikuwa na mechi 11 ambazo nilipata wakati mgumu kwa kutaniwa!
"Ninatumai ataendelea kubaki
England na kujaribu kuelewa kwamba huwezi kung'ata mkono wa mtu."
@@@@@@@@
Loic Remy kumrithi Suarez Liver
LIVERPOOL ipo tayari kutoa ofa ya pauni
milioni 8 kwa Mshambuliaji wa QPR, Loic Remy wakati huu ambao inajiandaa
kuingia msimu mpya bila Luis Suarez.
Liverpool bado inaamini kuwa haitaweza
kumzuia raia huyo wa Uruguay kutimka nje ya England katika usajili wa majira ya
joto.
Suarez, ambaye amefungiwa mechi 10 na
hivyo sasa kulazimika kukosa michezo yote iliyobaki msimu huu baada ya
kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, pia atakosa mechi sita za mwanzo
za msimu ujao.
@@@@@@@@
Spurs yamtaka Soldado wa Valencia
Tottenham imepiga
hatua katika mpango wao wa kutaka kumsajili Mshambuliaji wa Kihispania, Roberto
Soldado wakati huu ambao Mwenyekiti wao, Daniel Levy akitaka kumtafutia
wasaidizi Gareth Bale ili kuweza kutoa upinzani wakutosha msimu ujao.
Spurs ilitarajiwa kuwa kati ya
watazamaji ambao wangehudhuria mechi kati ya Valencia na Real Sociedad, lakini
lengo lao likiwa ni kumtazama Soldado, 27 wa Valencia.
@@@@@@@@
Wenger amtaka Iker Casillas
Arsene Wenger anamatumaini makubwa ya kuimiliki huduma ya
Kipa namba moja wa Hispania, Iker Casillas na tayari amemweka kama chaguo lao
namba moja kuelekea usajili wa majira ya joto, limeandika Gazeti la the Sunday
People.
Kipa huyo wa Real Madrid hakubaliki na
Kocha wa miamba hiyo ya Bernabeu, Jose Mourinho na kabla ya mechi ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya dhidi ya Dortmund wiki iliyopita ambayo alicheza na kuruhusu
mabao manne, alikuwa hajachezeshwa tangu Januari.
Kocha wa 'Gunners', Wenger amejaribu
kurusha ndowana kama anaweza kupata saini ya kipa huyo, 31, ambaye hajawahi
kucheza klabu nyingine tangu aanzie soka lake Ashburton Grove.
@@@@@@@@@@@
Jovetic awekwa kiporo Fiorentina
RAIS wa Fiorentina, Mario Cognigni
amekiri kwamba ofa nyingi zinatarajiwa kutua kwa mshambuliaji wao, Stevan
Jovetic. Mshambuliaji huyo ni mmoja kati ya wachezaji wanaowindwa sana na
Arsenal.
"Jovetic ni mwenye furaha hapa
Florence,” Cognigni alisema. “Kama tulivyosema mwanzoni, tutakaa naye na
kujadili mustakabali wake wa baadaye mwishoni mwa msimu.
“Lakini, hadi sasa, Jovetic ataendelea
kufikiria kuhusu Fiorentina tu.”
@@@@@@
Wiki muhimu kwa Kaizer Chiefs
JOHANNESBURG,
Afrika Kusini
KAIZER
Chiefs jana ilianza wiki muhimu ambayo ndiyo itakuwa na mechi mbili zitakazotua
mwanga kwa timu hiyo, kama itatwaa ubingwa wa soka nchini Afrika Kusini mapema
au italazimika kusubiri hadi dakika za mwisho.
Chiefs
jana ilikuwa kibaruani ikiwakaribisha moja ya wapinzani wao katika mbio za
kuwania ubingwa huo, Platinum Stars katika mchezo ambao ni muhimu kwa timu zote
hasa kwa kuwa Chiefs walihitaji ushindi ili kujiimarisha kileleni, lakini
Platinum walihitaji ushindi ili kupunguza pointi.
Platinum
wana pointi 49 katika nafasi ya pili huku Chiefs wakiwa kileleni kwa kuwa na
pointi 55, hivyo pambano hilo lilikuwa na umuhimu mkubwa kwa timu zote mbili
kushinda kwa kila mmoja ingenufaika zaidi na ushindi katika mechi hiyo.
Mbali na
mchezo huo, mechi nyingine muhimu kwa
Chiefs ni ile ya mahasimu wao wa jadi Orlando Pirates, ambayo itacheza na
Chippa united hapo kesho, ambapo endapo
Pirates watapoteza au kutoka sare basi ni wazi kwamba, Chiefs watakuwa na
nafasi kubwa ya kutawazwa mabingwa wapya wa soka nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment