RAIS SAMIA KUTUNUKU WASHINDI WA TUZO ZA SAMIA KALAMU 2026 DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Uandishi wa Habari za Maendeleo (Samia Kalamu Awards 2026) itakayofanyika tarehe 5 Desemba 2026 katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo itashuhudia utoaji wa tuzo kwa waandishi wa habari 64 na vyombo vya habari 11 vilivyofanikiwa kufuzu hatua ya mwisho ya kinyang'anyiro hicho.
Taarifa hiyo kuhusu tuzo hizo imetolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Rolf Kibaja, imebainisha kuwa jumla ya kazi 3,003 ziliwasilishwa kuwania tuzo hizo, ambapo baada ya tathmini ya awali ya majaji, kazi 882 zilifuzu kupigiwa kura na umma na kufanikisha kupatikana kwa jumla ya kura 317,399.
Mchakato wa kupata waliofuzu hatua hiyo ya mwisho umehusisha tathmini kutoka kwa majaji 19 pamoja na kura za wananchi. Majaji walizingatia vigezo mbalimbali ikiwemo ubora wa maudhui, uzingatiaji wa maadili ya taaluma, matumizi ya utafiti na takwimu, athari chanya kwa jamii, pamoja na mchango wa kazi hizo katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Kategoria za tuzo hizo zimejumuisha Tuzo Maalumu za Kitaifa kama vile Chombo cha Habari Mahiri cha Kitaifa, Mwandishi Mahiri wa Nishati Safi ya Kupikia, na Mwandishi wa Habari Mahiri wa Jumla. Kwa upande wa Vyombo vya Habari, tuzo zinawania maeneo ya Chombo cha Habari Mtandaoni, Magazeti, Redio za Kijamii, Redio za Kitaifa na Televisheni, ambapo vyombo vinatakiwa kuwasilisha machapisho matano.
Pia, kipo kipengele kipana cha Tuzo za Kisekta na Umaharifa kinachohusisha zaidi ya kategoria 40. Kategoria hizo zinajumuisha Afisa Habari Mahiri wa Serikali, Mwandishi Mahiri wa Habari za Picha (unaohitaji machapisho 5), Mchoraji Mahiri wa Katuni, Mwandishi Mahiri wa Tahariri, pamoja na waandishi mahiri wa sekta mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar kama vile Afya, Ardhi, Elimu, Kilimo, Maji, Maliasili na Utalii, Vijana, na Utamaduni na Michezo. Sekta zingine ni pamoja na Diplomasia, Fedha na Uchumi, Jinsia, Kazi na Ajira, Madini, Mazingira, Nishati, Sheria, Siasa, TEHAMA, Uchukuzi, Uchumi wa Buluu, Ujenzi, Usalama wa Raia, Utawala Bora, Uwezekaji, Viwanda na Biashara, pamoja na Watu wenye Ulemavu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Dkt. Rose Reuben, amefafanua kuwa uteuzi wa washindani hao ulizingatia ubora wa kazi na vigezo vilivyowekwa wazi kwenye tovuti rasmi ya tuzo hizo wakati wa kutangaza nafasi ya kushiriki. Ameongeza kuwa Kamati ya Maandalizi itawapa maelekezo zaidi waliofuzu kuhusiana na ushiriki wao katika hafla hiyo ya utoaji wa tuzo.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amewashukuru waandishi kwa kushiriki na kuwasisitiza kuendelea kuzingatia maadili, weledi na uwajibikaji ili kuimarisha imani ya jamii kwa vyombo vya habari. Amebainisha kuwa tuzo hizi zinatoa fursa muhimu ya kutambua ubora wa kazi za waandishi, maafisa habari pamoja na vyombo vya habari.
Tuzo za Samia Kalamu zinaratibiwa na TCRA kwa kushirikiana na TAMWA na JAB, zikiwa zilianzishwa mwaka 2024 kwa lengo la kutambua na kuhamasisha ubora, weledi na ubunifu katika uandishi wa habari za maendeleo. Baada ya hafla ya kwanza kufanyika mwaka 2025, msimu huu wa pili unaendeshwa chini ya kaulimbiu isemayo “Kalamu kwa Maendeleo.”
Waandishi wa Habari Waliofuzu Kuwania SKA-2026
|
NA |
JINA |
CHOMBO CHA HABARI |
|
1. |
Adela Madyane |
TBC |
|
2. |
Rajabu
Mustafa Mrope |
Pangani
FM |
|
3. |
Jamaldini
Abuu Zuberi |
TBC |
|
4. |
Jesse
Mbezi Mikofu |
Mwananchi
|
|
5. |
Nusra
Shaaban Juma |
Zanzibar
Leo |
|
6. |
Sanula
Renatus Athanas |
Nipashe
|
|
7. |
Christine
Stephen Mwakangale |
The
Guardian Ltd |
|
8. |
Julius
M Maricha |
The
Citizen |
|
9. |
Rahma
Suleiman Ali |
Nipashe
|
|
10. |
Mnaku
Bernard Mbani |
The
Guardian Ltd |
|
11. |
Joseph
Ernest Nakajumo |
Uhuru
Publications Ltd |
|
12. |
James
Albert Kandoya |
The
Guardian Ltd |
|
13. |
Halfan
Ramadhani Chusi |
Nipashe
|
|
14. |
Riziki
Abdalla Ali |
Zanzibar
Leo |
|
15. |
Esco
Donald Mkandawile |
Simulizi
na Sauti |
|
16. |
Emmanuel
Bwighane Kalemba |
Azam
Media |
|
17. |
Elesia
Thomas Haule |
Azam
Media |
|
18. |
Maregesi
Evarist Paul |
Pambazuko
Newspaper |
|
19. |
Aveline
Kitomary |
TSN |
|
20. |
Rosemary
Joseph Mirondo |
The
Citizen |
|
21. |
Yusuph
Michael Mazimu |
BBC |
|
22. |
Mussa
Yusuph Mussa |
Uhuru |
|
23. |
Isack
Dickson Lukumay |
Orkonerei
FM |
|
24. |
Gervas
Charles Mwatebela |
TBC |
|
25. |
Saada
Amir Mlagwa |
Mwananchi
|
|
26. |
Beatrice
Moses Kabojoka |
The
Guardian |
|
27. |
Rahel
Japhet Pallangyo |
Habari
Leo |
|
28. |
Mathias
Said |
Wazohuru
Media |
|
29. |
Khamisuu
Abdallah Ali |
Zanzibar
Leo |
|
30. |
Baraka
Loshilaa |
Mwananchi
|
|
31. |
Asya
Hassan Bakar |
Zanzibar
Leo |
|
32. |
Gwamaka
Mwaipungu Alipipi |
Nipashe
|
|
33. |
Emmanuel
Omondi Onyango |
The
Guardian |
|
34. |
Ramadhani
Ismail Nyassa |
The
Citizen |
|
35. |
Josephine
Sebastian |
The
Citizen |
|
36. |
Esther
Assimwe |
TBC |
|
37. |
Beatrice
Philemon Mukocho |
The
Guardian |
|
38. |
Vuai
Makame |
Tumbatu
FM |
|
39. |
Neema
Emmanuel Abel |
Nipashe
|
|
40. |
Gadiosa
Lamtey |
The
Citizen |
|
41. |
Aurea
Simtowe |
Mwananchi
|
|
42. |
Sameer
Ahmed |
TBC |
|
43. |
Ngarayai
Ole-Kimosa |
TBC |
|
44. |
Innocent
Anselemi |
Tumaini
Media |
|
45. |
Simon
Mkina |
Pambazuko
|
|
46. |
Fatma
Chikawe |
Azam
Media |
|
47. |
Eliya
Marohe |
Mwananchi
|
|
48. |
Ally
Mbogo Mayala |
TSN |
|
49. |
Maureen
Minanago |
TBC |
|
50. |
Ahmada
Juma |
The
Daily News |
|
51. |
Daniel
Samson |
Nukta
Africa |
|
52. |
Rose
Yolam Masaka |
TBC |
|
53. |
David
Katimbila Geke |
TBC |
|
54. |
Shaban
Hamisi Njia |
Nipashe
|
|
55. |
Tuma
Dandi |
TBC |
|
56. |
Albano
Maganga Midelo |
Habari
Leo |
|
57. |
Harith
Ally |
Watetezi
Tv |
|
58. |
Esau
Ng'umbi |
Nukta
Africa |
|
59. |
Marco
Zephania Maduhu |
Nipashe
|
|
60. |
Bakari
Chijumba |
Ayo TV |
|
61. |
Ichikael
Leonard Malisa |
Afisa
Habari - Njombe |
|
62. |
Adam
Gabriel Hhando |
Afisa
Habari - Tanga |
|
63. |
Albano
Maganga Midelo |
Afisa
Habari - Ruvuma |
|
64. |
Francis
Kajubi |
The
Guardian Ltd |
Vyombo vya Habari Vilivyofuzu Kuwania SKA-2026
|
NA. |
VYOMBO VYA HABARI |
|
1. |
Azam 4
HD |
|
2. |
Safari
Channel |
|
3. |
Orkonerei
FM |
|
4. |
Mpanda
FM |
|
5. |
Mlimani
FM |
|
6. |
Mwananchi
|
|
7. |
Nipashe
|
|
8. |
Uhuru |
|
9. |
Habari
Leo |
|
10. |
The
Citizen |
|
11. |
Mlimani
TV |
Post a Comment