TANZANIA,UGANDA ZAKUBALIANA KUONDOA VIKWAZO CHA KIBIASHARA
Serikali za Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda zimekubaliana kwa pamoja kuharakisha
utatuzi wa vikwazo vyote vya biashara
Makubaliano haya muhimu
yamefikiwa leo tarehe 18 Novemba 2026 katika Ikulu ya Entebbe nchini Uganda
Katika mazungumzo
yao rasmi
"Tanzania itaendelea kushirikiana na Uganda
kwa moyo wa watu wamoja, hatima moja. Sasa ni wakati wa kuharakisha utekelezaji
wa tuliyokubaliana," Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan
Rais Dkt. Samia pia
ameipongeza Uganda kwa hatua yake ya kihistoria ya kuwa Taifa la kwanza kuanza
ujenzi wa ubalozi wake katika Mji wa Serikali jijini Dodoma tangu kuzinduliwa
kwa mji huo
Kwa upande wake, Rais
Yoweri Kaguta Museveni amesisitiza umuhimu wa biashara kati ya nchi hizo mbili
kuzingatia mahitaji ya pamoja
"Tunahitaji maliasili, uzalishaji wa bidhaa,
soko la kutosha na mawasiliano," Rais Yoweri Kaguta Museveni
Viongozi hao
wawili wamejadili pia maendeleo ya miradi mikubwa ya kimkakati
Rais Museveni
ameeleza kuwa nchi yake inapanga kujenga kiwanda kidogo cha kusafisha mafuta
mkoani Hoima
Taarifa rasmi iliyotolewa
na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari S. Machumu, imesema
viongozi wote wawili wamehimiza utekelezaji wa haraka wa makubaliano yote
yaliyofikiwa
Post a Comment